|
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, amewapangua wakurugenzi wa idara mbalimbali ndani ya wizara yake lengo likiwa kuboresha ufanisi ndani ya wizara hiyo. Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Dk Mwakyembe alisema , kubadilisha watendaji ni mchakato ambao upo serikalini na hata hivyo waliokuwa katika nafasi hizo walikuwa wakikaimu. "Tumeweka wahusika kamili kwa nafasi zao, tunataka kuleta ufanisi wa utendaji ndani ya Wizara," alisema Mwakyembe. Katika panguapangua hiyo, Wakurugenzi wakuu na wasaidizi 14 ndiyo waliokumbwa na hatua hiyo. Taarifa ya Wizara iliyotiwa saini na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Omar Chambo, imewataja walioteuliwa kuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa miundombinu na usafiri, Mhandisi Edwino Mujwahuzi. Wengine walioteuliwa na nafasi zao kwenye mabano ni Peter Lupatu (Idara ya huduma na usafirishaji) na Gabriel Migire atakayeongozaiIdara ya Ssra na mipango. Pia yumo Festo Mwanyika (Mkurugenzi msaidizi, huduma za usafiri wa reli) na Aron Kisaka atakayekuwa Mkurugenzi msaidizi, huduma ya usafiri wa barabara. Deogratius Mukasa atakuwa Mkurugenzi msaidizi wa huduma za safiri wa majini wakati Hilal Ali Mohamed ameteuliwa wadhifa wa Mkurugenzi msaidizi miundombinu ya reli. Wengine ni Injinia Rugera Majula (Mkurugenzi msaidizi, miundombinu ya Viwanja vya Ndege) na Aminel Hassan Omar aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi msaidizi wa miundombinu ya bandari. Chambo aliwataja wengine kuwa ni Erasto Wapalila (Mkurugenzi msaidizi wa ulinzi na usalama wa usafirishaji na Aunyisa Meena atakayekuwa Mkurugenzi msaidizi wa usimamizi, ufuatiliaji na tathimini. Wengine walioteuliwa kwa mujibu wa taarifa hiyo ni Sifael Sekei (Mkurugenzi msaidizi, mazingira na huduma za jamii) na Edward Mkiaru anayekuwa Mkurugenzi msaidizi wa sera. Aidha katika uteuzi huo, Abdulrahaman Said Mbamba ameteuliwa kuwa Mkuu wa kitengo cha teknolojia ya habari na mawasiliano. “Tumeteua wakurugenzi na wakurugenzi wasaidizi wapya kwa lengo la kuimarisha utendaji katika wizara hiyo, wananchi watarajie ufanisi bora wa kazi,î ilisema sehemu ya taarifa hiyo. Mabadiliko hayo yamekuja ikiwa ni miezi minne tangu Dk Mwakyembe amsimamishe kazi bosi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), Paul Chizi kutokana na tuhuma za ufisadi. Aidha mabadiliko hayo yamekuja ikiwa ni miezi miwili na nusu tangu Dk Mwanyembe amsimamishe kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraem Mgawe kutokana na matumizi mabaya ya ofisi yake. |
Monday, October 15, 2012
Mwakyembe apangua wakurugenzi uchukuzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment