Friday, December 7, 2012

Wednesday, December 5, 2012

CCM haiwezi kupambana na rushwa – Msigwa






MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) hakitaweza kufanikiwa kupambana na kuzuia rushwa nchini, kutokana na viongozi wengi wa chama hicho kupatikana kwa njia ya rushwa.
Msigwa aliyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika viwanja vya Mwembetogwa mkoani hapa.
Mbali na Msigwa kuinyooshea kidole CCM kwa rushwa, Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi CHADEMA, Msafiri Mtemelwa, alisema wakati wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, chama hicho tawala hakikuwa kama kilivyo sasa.
Alisema CCM ilikuwa ina maadili mema, lakini hivi sasa kila kona nchini imejaa rushwa ambayo inasababisha adha kubwa kwa maskini.
Aliongeza kuwa licha ya michakato mbalimbali ya kukibadili chama kwa maana ya viongozi kama njia ya kukisafisha, wamekuwa wakisahau kuwa wanaowapatia uongozi ni watu ambao tayari walishaiingiza nchi pabaya.
“Leo mmeambiwa viongozi wa CCM wamewabadilisha! Wamewabadilishieni kanzu lakini mapadre au mashehe ni wale wale, Kinana ambaye aliaga siasa basi anastaafu, leo amerudi kufuata nini?” alisema Mtemelwa.
Akitolea mfano kwa baadhi ya viongozi ambao wameipeleka nchi pabaya, alimtaja aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Philip Mangula, akiwa na mwenyekiti wake Benjamin Mkapa akidai kuwa walichangia kwa kiasi kikubwa kuiyumbisha nchi.
“Mkapa na Mangula ndio walioifilisi nchi hii. Mangula aliuza nyumba za serikali akiwa Katibu Mkuu na Mwenyekiti akiwa Mkapa. Mangula pia aliuza machimbo ya almasi katika nchi hii yeye akiwa Katibu Mkuu na Mwenyekiti akiwa Mkapa,” alisema.
Hata hivyo alidai kuwa Mwalimu Nyerere aliacha machimbo ya madini maeneo mawili, Buhemba na Shinyanga Mwadui, lakini Rais Jakaya Kikwete na wenzake wameuza North Mara Lyamungo pamoja na Buhemba mkoani Mara huku wananchi wakiendelea kulia njaa.
Alieleza kuwa taifa la Tanzania ni taifa tajiri duniani kuliko sehemu nyingine yoyote isipokuwa linakosa viongozi wenye maadili bora wa kusimamia rasilimali hizo kwa manufaa ya taifa.
Aidha amewataka Watanzania hususan vijana kuchukua hatua za haraka za kuchagua viongozi makini ili kuinusuru nchi kutoka mikononi mwa viongozi wanaofanya kazi kwa maslahi binafsi na kuhakikisha Kikwete ndiye Rais wa mwisho nchini kutoka CCM.

Mnyika apeleka hoja ya maji Halmashauri


MBUNGE wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA), John Mnyika, jana aliwasilisha katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam hoja binafsi inayohusu uboreshaji wa huduma ya majisafi na uondoaji wa majitaka katika maeneo mbalimbali jijini.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, iliyotumwa na Katibu wa Mbunge Aziz Himbuka, alisema lengo la hoja hiyo ni kupendekeza baraza la madiwani wa jiji, kujadili na kupitisha maazimio ya hatua za haraka zaidi za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jimbo la Ubungo na jiji katika masuala yaliyo chini ya mamlaka ya halmashauri.
Mnyika alisema ameamua kuchukua hatua hiyo wakati huu ili Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iweze kutimiza wajibu wake mwezi huu, huku akisubiri kuwasilisha hoja binafsi bungeni katika mkutano wa kumi Februari 2013 endapo Wizara ya Maji haitachukua hatua zinazostahili.
Alisema pamoja na mafanikio ya kawaida yaliyopatikana kupitia mikutano yake na wananchi katika kata mbalimbali jimboni kwake, ufuatiliaji serikalini bado una matatizo yanayohitaji baraza la madiwani kushughulikia kwa ajili ya Jimbo la Ubungo na Mkoa mzima wa Dar es Salaam.
Mbunge huyo alisema kufuatilia masuala ya maji, alianza kwa kufanya kongamano la Maji katika Jimbo la Ubungo mwanzoni mwa mwaka 2011 ili kuwakutanisha wananchi, mamlaka husika na wadau wengine katika kuunganisha nguvu kupata ufumbuzi.
Alizitaja hatua nyingine ambazo amekwishazichukua ili ziweze kufanyiwa haraka ni pamoja na kuishirikisha DAWASA, DAWASCO na Wizara ya Maji ambao alidai utekelezaji wao ulikuwa mdogo na kwamba mpaka sasa hakuna ambacho kimeishafanyika.
Hivyo, Mnyika alisema kutokana na hilo aliamua kukusanya nguvu ya pamoja kufanya maandamano ya kudai maji hadi katika ofisi kuu za DAWASCO.
“Maandamano hayo yalizaa matunda kwa upande wa DAWASCO ambapo ameshafanya nao ziara ya kikazi ya kata mbalimbali ya kutembelea maeneo yenye matatizo na hatua zimechukuliwa ambazo zimewezesha baadhi ya maeneo kuanza kutoka maji,” ilisema taarifa yake.
Hata hivyo alisema bado yapo maeneo mengi yenye matatizo makubwa ya maji ikiwemo ya Msumi, Makabe, Msakuzi, Malambamawili, Msingwa, Goba na mengineyo mengi katika jiji la Dar es salaam.

Petroli bei juu






MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo ya bidhaa za mafuta ya petroli nchini ambayo imeongezeka kwa sh 70 kwa lita sawa na asilimia 3.4.
Hatua hiyo ni wazi kuwa itasababisha gharama za nauli kuwa juu, pamoja na usumbufu kwa abiria katika nyakati hizi za kuelekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Anastas Mbalawa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Haruna Masebu, alisema kuwa bei hizo zitaanza kutumika kuanzia leo na kuwataka wamiliki wa vituo vya mafuta kutambua bei kikomo ya bidhaa hizo.
Taarifa hiyo ilitaja bei hizo katika Jiji la Dar es Salaam kwa petroli itakuwa sh 2,119, dizeli sh 1,999 na mafuta ya taa sh 2,023; Arusha petroli sh 2,203, dizeli sh 2,083 na mafuta ya taa sh 2,107 huku Dodoma petroli itauzwa sh 2,146, dizeli sh 2,058 na mafuta ya taa sh 2,082.
Mkoani Iringa petroli itauzwa kwa sh 2,183, dizeli sh 2,063 na mafuta ya taa sh 2,087, huku Morogoro petroli itauzwa kwa sh 2,144, dizeli sh 2,024 na mafuta ya taa sh 2,048 na Bukoba petroli sh 2,334, dizeli sh 2,214 na mafuta ya taa sh 2,238.
Alisema kuwa bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote ya petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la Novemba 7, 2012.
“Katika toleo hili, bei za rejareja kwa dizeli imeongezeka sh 10 kwa lita sawa na asilimia 0.53, bei ya mafuta ya taa imepungua kwa sh 3 kwa lita sawa na asilimia 0.1, huku bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimeongezeka petroli kwa sh 69.56 kwa lita sawa na asilimia 3.52; dizeli kwa sh 10.04 kwa lita sawa na asilimia 0.52,” alisema.
Alisema kuwa bei ya mafuta ya taa imepungua kwa sh 3 kwa lita sawa na asilimia 0.15 huku akisema kuwa mabadiliko ya bei hizo yametokana na ongezeko la bei ya mafuta katika soko la dunia na kushuka kidogo kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani.
Mbalawa alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko ambapo EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa hizo.
“Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na fomula mpya iliyopitishwa na mamlaka yetu na kuchapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 la Desemba 23, 2011,” alisema.
Aidha, alisema kuwa ni muhimu vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei za bidhaa hizo katika mabango yanayoonekana, huku ikionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.
Alisema kuwa ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja, na kwamba adhabu itatolewa kwa kituo husika.

Dk. Slaa, Nape jino kwa jino






KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema anampongeza Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa, kwa kukiri kwamba anamiliki kadi ya CCM hadi leo.
“Kwanza nampongeza kwa kuanza kujifunza kusema ukweli maishani mwake, bila shaka ametambua kuwa uongo haulipi. Kitendo cha kukiri anamiliki kadi ya CCM bado ni cha kiungwana, nampongeza kwa hili,” alisema Nape, baada ya mwandishi wetu kumtaka maoni yake juu ya Dk. Slaa kukiri kumiliki kadi ya CCM hadi sasa.
Akijibu tuhuma za Nape alizotoa juzi kwamba baadhi ya vigogo wa CHADEMA akiwemo Dk. Slaa, bado wana kadi za CCM na baadhi yao wanaendelea kuzilipia, Katibu huyo wa CHADEMA kupitia vyombo vya habari, amekiri kuwa anayo kadi ya CCM na kwamba anaitunza kama kumbukumbu muhimu kwake.
Pia Dk. Slaa alisema Nape anapiga mayowe na kumtaka asiwapotezee muda Watanzania kwa kujadili mambo yasiyo na msingi na kuacha kujadili suala la umaskini na jinsi ya kuwasaidia kuondokana na hali hiyo.
Pamoja na pongezi hizo, Nape amemtaka Dk. Slaa kuwaambia Watanzania kwamba kadi hiyo ameilipia mpaka lini, pia aache tabia ya kuwadanganya wenzake kurudisha kadi zao za CCM huku yeye akibaki na yake kibindoni.
“Ni vizuri sasa Dk. Slaa awaambie Watanzania amelipia mpaka lini kadi hii. Lakini aache kuwadanganya wenzake kurudisha kadi zao huku yeye akibaki na yake huu ni unafiki,” alisema Nape.
Aidha Nape ambaye amekiri kumheshimu sana Dk. Slaa kama Babu yake, amesema alishtuka sana kusikia Katibu Mkuu huyo wa CHADEMA akiwatuhumu viongozi wa chama hicho, hivi karibuni kuwa ni mamluki wa CCM huku akijua yeye ni mamluki namba moja kwani wenzie hawana kadi za CCM yeye anayo.
“Nimesikia anahoji hili linawasaidiaje Watanzania maskini! Swali hili limethibitisha upeo mdogo sana wa kufikiri wa kiongozi mkubwa na ninayemheshimu kama huyu. Lazima ajue kwamba yeye anaomba kuwa kiongozi, hivyo lazima wananchi tumjue tabia zake,” alisema Nape na kuongeza:
“Viongozi wanafiki wa aina yake ni janga kwa taifa letu.Usipokuwa mwaminifu kwa kidogo huwezi kuwa mwaminifu kwa kikubwa. Lazima anayetaka kuwa kiongozi aishi anayoyasema.”

Lema atoa sababu 18 kutetea ubunge wake






ALIYEKUWA Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbles Lema, amewasilisha sababu 18, kuiomba Mahakama ya Rufaa nchini, itengue hukumu ya awali iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili mwaka huu ambayo ilifuta ubunge wake.
Ombi hilo liliwasilishwa mahakamani hapo jana na mawakili wa Lema, Method Kimomogoro na Tundu Lissu ambao walidai kuwa hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalila haina hadhi ya kuitwa hukumu.
Mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa linaloongozwa na Jaji Natharia Salum Massati, wakili Kimomogoro, alieleza mahakama kuwa rufaa ya mteja wake ina jumla ya sababu 18 za kupinga hukumu iliyotolewa na Jaji Rwakibalila.
Katika hukumu yake iliyoibua mjadala mkubwa nchini Aprili mwaka huu, Jaji Rwakibalila alimtia hatiani Lema kwa makosa ya kutoa lugha za kumkashifu mgombea mwenzie, Dk. Batilda Buriani (CCM) na kumfungia kutogombea ubunge kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo.
Alidai kuwa, Jaji Rwakibalila alijielekeza vibaya katika hukumu yake alivyosema kuwa kesi za uchaguzi hazitawaliwi na kanuni za sheria za Uingereza kwani kuna maamuzi ya kesi mbalimbali yaliyokwishatolewa na Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu nchini na kuruhusu kesi za uchaguzi ziamuliwe kwa kutumia kanuni na sheria za Uingereza.
Katika hoja ya pili, Kimomogoro alidai kuwa Jaji Rwakibalila alijielekeza vibaya kuruhusu wajibu rufaa, wasitaje maneno kwenye hati ya madai ambayo walidai ni maneno ya udhalilishaji wa kijinsia na dini ambayo yanadaiwa kutolewa na Lema, kwenye mikutano ya kampeni dhidi ya Dk. Burian.
Hoja nyingine ni kwamba hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kwamba wajibu rufaa kama kweli waliandikishwa kupiga kura katika Jimbo la Arusha Mjini mwaka 2010 au la.
Kwa mujibu wa wakili huyo, hoja nyingine ni kwamba Jaji Rwakibalila alikosea kisheria kusema kuwa mtu yeyote akiwemo mpiga kura ana haki ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo ambalo yeye ni mpiga kura na kuongeza kuwa, wao wanaomba Mahakama ya Rufaa itamke kuwa wajibu rufaa (wapiga kura wa Jimbo la Arusha waliofungua kesi ile), hawana haki kisheria kufungua kesi ile ya kupinga ubunge wa Lema kwani mwenye haki ya kufanya hivyo ni Dk. Batilda mwenyewe.
Aliongeza kuwa, mpiga kura yeyote hana haki ya kufungua kesi ya kupinga ubunge wa Arusha Mjini kwani haki zao hazikuvunjwa.
Aidha, katika hoja nyingine alidai kuwa Jaji Rwakibalila hakutumia maamuzi ya kesi za Mahakama ya Rufaa wala vifungu vya sheria ambavyo mawakili wa pande zote mbili waliziwasilisha mbele yake katika majumuisho yao ya mwisho.
Alidai kuwa, maamuzi ya Mahakama ya Rufaa katika kesi zile yalisisitiza kuwa lazima kesi ithibitishwe bila kuacha mashaka yoyote, lakini katika hukumu ya Lema, Jaji Rwakibalila imeacha mashaka mengi, ndiyo maana Lema anadai jaji huyo alikosea.
Baada ya wakili Kimomogoro kuwasilisha hoja hiyo iliyodai Jaji Rwakibalila hakutumia maamuzi ya kesi zilizowasilishwa mbele yake na mawakili wa pande mbili, Jaji Massati alisema si lazima jaji au hakimu atumie kesi zilizowasilishwa mbele yake na mawakili katika kutoa uamuzi.
Hoja nyingine ni kwamba, hukumu ya Lema iliegemea katika ushahidi wa mdomo tu bila kuwepo ushahidi wa kuunga mkono kwani mashahidi wa mjibu rufaa, waliotoa ushahidi walidai walimsikia Lema katika mikutano ya kampeni akitoa maneno ya kumdhalilisha na kumkashfu Dk. Batilda, lakini walishindwa kuleta CD, mikanda ya video kuthibitisha.
“Tulimueleza Jaji Rwakibalila kuwa mashahidi wa wajibu rufaa hawaaminiki na kwamba ushahidi wao ulikuwa wa mazingira, lakini jaji katika hukumu yake hakuna sehemu aliyoonyesha kukubali wala kukataa hoja yetu hii,” alidai wakili Kimomogoro.
Wakili huyo alidai pia Jaji Rwakibalila alikosea alivyosema Lema ana bahati kwani hakukamatwa wala kushitakiwa kwa kutoa lugha za kashfa na udhalilisha katika mikutano ya kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010.
Kutokana na madai hayo, alidai kuwa Lema anaiomba Mahakama ya Rufaa itamke kuwa Jaji Rwakibalila alitamka neno hilo kwa bahati mbaya na kutamka kwake neno hilo ndiko kulikomsukuma kufikia uamuzi wa kumfungia Lema asigombee kwa kipindi cha miaka mitano.
“Kwa hoja hizo tulizoziwasilisha hapo juu, tunaiomba Mahakama ya Rufani nchini itengue hukumu ya Jaji Rwakibalila kwani haina vigezo wala hadhi ya kuifanya iwe hukumu, na pia tunaiomba mahakama iwaamuru wajibu rufaa walipe gharama za uendeshaji wa kesi hiyo tangu ilipoanza Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na sasa Mahakama ya Rufaa,” alidai wakili Kimomogoro.
Kwa upande wake wakili wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Uchaguzi, Timon Vitalis, alidai kuwa sheria ya uchaguzi haiwaruhusu wapiga kura kufungua kesi ya kupinga ubunge wala wagombea ubunge, udiwani kwani aliyepaswa kufungua kesi hiyo ni Dk. Batilda na siyo wajibu rufaa ambao ni wapiga kura wa Jimbo la Arusha Mjini.
Hata hivyo hoja hizo zilipanguliwa na mawakili wa wajibu rufaa, Aluthe Mugwai na Modest Akida na Wakili wa Msimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Vitalis.
Mugwai na Akida walitetea kuwa hukumu ile ni sahihi na haistahili kutenguliwa kwani imekidhi matakwa ya kisheria na kuomba mahakama hiyo itupilie mbali rufaa ya Lema.
Mugwai alisema mawakili wa Lema wanaipotosha mahakama kwa kusema hakukuwa na uthibitisho wowote ulioonyesha wajibu rufaa walikuwa wapiga kura wa Jimbo la Arusha Mjini wakati ukurasa wa 10 katika hukumu inayopingwa, inaonyesha namba za vitambulisho vya wapiga kura ambavyo ni vya wajibu rufaa na wakati vikitolewa mahakamani, mawakili hao wa Lema walikuwepo.
Kuhusu hoja ya jaji kwamba alijielekeza vibaya kusema kuwa sheria za Uingereza hazitakiwi kutumika kuamua katika kesi za uchaguzi, Mugwai alidai Jaji Rwakibalila yupo sahihi kwani hata kifungu cha 1(2) cha sheria ya uchaguzi sura ya 343, kinasema masuala yote ya uchaguzi yatashughulikiwa kwa kutumia sheria ya uchaguzi na kuongeza kuwa mawakili wa Lema wametumia kesi za Mahakama ya Rufaa zilizoamriwa kwa sheria ya zamani ya uchaguzi ya mwaka 1985 wakati sheria hiyo ya uchaguzi imeishafanyiwa marekebisho na marekebisho ya mwisho yalifanyika mwaka 2010 .
“Hata kifungu cha 2 (3) cha sheria ya Judicuture and Application of Law (JALA), inakataza matumuzi ya sheria za nje kutumika kuamua kesi za uchaguzi wakati nchi yetu ina sheria mahususi ya uchaguzi kwa ajili ya kuamua kesi za uchaguzi na kwamba jaji alikuwa sahihi kusema hilo na pia alikuwa sahihi kusema wajibu rufaa walikuwa na haki ya kufungua kesi hiyo na kuongeza kuwa hoja hiyo ni butu,” alidai wakili Mugwai.
Hata hivyo, alipinga hoja ya mawakili wa Lema iliyodai Jaji Rwakibalila katika hukumu yake hakutumia kesi walizoziwasilisha mbele yake, ambapo alidai katika hukumu hiyo alitumia baadhi ya kesi walizoziwasilisha mbele yake na kwamba jaji ana mamlaka ya kuchuja kesi anazotaka kuzitumia kwenye hukumu.
Akijibu hoja kwamba hukumu ya Lema iliegemea kwenye ushahidi wa mazingira tu, wakili Mugwai alikanusha na kusema hakukuwepo ushahidi wa mazingira kwani mashahidi waliomsikia Lema akitoa maneno ya kashfa kwenye mikutano ya hadhara, walifika mahakamani hapo na kutoa ushahidi wao ambapo walisema walimwona na kumsikia akfanya hivyo dhidi ya Batilda.
Hata hivyo wakati wakili Mugwai akiwasilisha hoja zake, baadhi ya watu wanaodaiwa ni wafuasi wa CHADEMA ambao walijazana ndani ya chumba cha mahakama, waliguna na kutoa vicheko hali iliyosababisha wakili huyo awaombe majaji wawadhibiti watu wenye tabia hiyo kwani mawakili wa Lema walipokuwa wakiwasilisha hoja zao walitulia.
Rufaa hiyo inayovuta hisia za wengi ndani na nje ya nchi, ilianza kusikilizwa majira ya saa tatu asubuhi na kumalizika saa tisa alasiri.
Kesi hiyo imeahirishwa na sasa kinachosubiriwa ni tarehe ya hukumu ili kukata mzizi wa fitina.
Kwa mujibu wa jopo hilo la majaji wa Mahakama ya Rufaa, tarehe ya kutolewa uamuzi wa rufaa hiyo itatolewa kwa njia ya maandishi kwa mawakili wa pande zote mbili.

Saturday, October 20, 2012

MAONI YA FRANK LUPEKE

KANUNI KUMI ZA KUIKOMBOA TANZANIA KUTOKA KWA WAKOLONI WEUSI (CCM)
1. Usiwe msaliti kwa NCHI yako. kuwa MZALENDO
2. Usiwe MVIVU wa kufikiri. Kuwa MDADISI.
3. Usiwe Mwoga, WOGA WAKO NDIYO UMASKINI WAKO.
4. Toa maoni tupate KATIBA bora. Na hakikisha unajiandikisha kwenye DAFTARI LA WAPIGA KURA.
5. Usitoe wala Kupokea RUSHWA. RUSHWA NI ADUI WA HAKI.
6. Usiwe MROHO wa MADARAKA kama LOWASA na CUF.
7. Tambua WAJIBU na HAKI zako. Hasa ya KUPIGA KURA.
8. Usiwasikilize WAGOMBEA na VIONGOZI wa CCM, Maana WATAKULAGHAI.
9. Usiwe na TAMAA ya vitu kama KANGA, KOFIA, TSHERT, VILEMBA na UBWABWA wa CCM.
10. (Amri Kuu)
Usimpigie KURA mgombea Yeyote wa CCM katika UCHAGUZI wowote ule kuanzia MWENYEKITI wa KIJIJI/MTAA, DIWANI, MBUNGE na RAIS.

MUNGU WAFUNGUE WATANZNIA, MUNGU IBARIKI TANZANIA

‘Maoni ya wananchi ni muhimu katiba mpya’





MWENYEKITI wa Mtandao wa Asasi za Kiraia Mkoa Lindi (LANGO), Mudhihiri Mewile, amewataka wakazi wa Somanga kutumia fursa zilizopo za kutoa maoni ya katiba ili nchi ipate katiba yenye kujali maslahi ya taifa na si ya wanasiasa.
Akizungumza kwenye mdahalo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya katiba uliofanyika jana kwenye Jimbo la Kilwa Kaskazini, Mawile aliwataka wananchi kutoogopa kutoa maoni katika katiba mpya, kwani ni mali yao.
Katika mdahalo huo uliofanyika katika maeneo ya Kijiji cha Somanga, wananchi wengi walijitokeza kutoa maoni ambapo Ally Mohamedi alitaka katiba ijayo iangalie masilahi ya wazee kwani ndio waliochangia mapato ya nchi hii.
Husna Seleman alitaka suala la elimu ya vitendo mashuleni kuanzia shule ya msingi mpaka vyuoni lidhibitiwe na isiwe inafanyiwa mabadiliko ya mitaala mara kwa mara.
“Kwa upande wangu nilitaka suala la elimu kwa vitendo lianzie katika shule za msingi hadi vyuoni kwani itasaidia sana, itakapotokea mwanafunzi ameshindwa mitihani yake ataweza kujiajiri mwenyewe,” alisema Husna.

Ulimboka amefungua milango ya uchunguzi




VYOMBO vingi vya habari juzi vimetawaliwa na habari inayomhusu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka, ambaye ameweka bayana kile kilichomsibu usiku wa Juni 26 mwaka huu, katika msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Dk. Ulimboka ameeleza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwataja kwa majina baadhi ya watendaji wa Ikulu ambao anaamini kuwa walihusika kwa namna moja ama nyingine katika tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwake.
Tunampongeza Dk. Ulimboka kwa kuweka bayana kile anachokiamini kuwa ndiyo ukweli wa tukio la kutekwa kwake, kwani tunadhani sasa atakuwa amefungua milango ya sakata hilo kuchunguzwa kwa umakini kukata mzizi wa fitina.
Ni kweli kesi ya tukio hilo imefunguliwa mahakamani ambapo raia mmoja wa Kenya anashtakiwa kufanya tukio hilo, lakini bado haizuii uchunguzi wa kina kuendelea hasa wakati huu ambapo muhusika amejitokeza wazi kutoa ushirikiano wa kuwatambua wale waliomfanyia kitendo hicho.
Tume ya uchunguzi iliyoundwa na Jeshi la Polisi kuchunguza tukio hio, imekuwa ikinyooshewa kidole na baadhi ya wadau wakiwemo madaktari wenyewe kwa madai kuwa haiko huru kwani baadhi ya wajumbe wake ni watuhumiwa.
Hata Dk. Ulimboka katika taarifa yake hiyo ya jana, amesisitiza kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano wa kina endapo kitaundwa chombo huru kuchunguza tukio hilo.
Ni vyema serikali ikajitafakari upya ili kuondoa sintofahamu hii vinywani mwa watu kwa kuunda chombo huru ili kuchunguza sakata hilo na hivyo kumfanya Dk. Ulimboka na Watanzania wengine kujiona wana haki ya kuishi kwa amani katika nchi yao.
Dk. Ulimboka ameeleza wazi kuwa anathibitisha kwamba Ramadhani Ighondu alitambulishwa kwao kwa jina la Abeid. Kwamba Binafsi anamfahamu sana bwana huyu kwa sababu alikuwa akitumwa mara kwa mara kuja kukutana naye na wamekutana mara kadhaa kabla ya tukio lile.
Alisema wazi kuwa anakumbuka kuwa Abeid alitambulishwa kwao na kigogo mmoja, akiwa pamoja na wawakilishi wengine wa madaktari kuwa yeye (Ramadhani Ighondu) ndiye atakayehusika katika kuchukua madai na hoja za madaktari katika mgogoro kati ya madaktari na serikali.
Kwamba anathibitisha kwamba mfanyakazi huyu wa Ikulu, ndiye aliyempigia simu na kumuita kwenye kikao ambako muda mfupi baadaye alitekwa. Katika mawasiliano hayo, Abeid alikuwa anatumia simu namba 0713 760473.
Dk. Ulimboka amebainisha kwamba hakuna shaka kwamba anamtambua Abeid kwa sura na namba aliyokuwa anatumia kuwasiliana naye mpaka siku ya kutekwa kwake.
Hivyo, kwa maelezo hayo ya Dk. Ulimboka, hatuhitaji kuibua mijadala ya malumbano ya nani kafanya nini na nani hakuhusika, isipokuwa jambo la msingi hapa ni kuundwa chombo huru kitakachokuja na majibu ya kumaliza utata huu, ndiyo maana tunasema Dk. Ulimboka amefungua milango ya uchunguzi.

DK. HELEN BISIMBA: Mwanaharakati mtetezi wa haki za binadamu




HELEN Kijo Bisimba, ni jina linalosikika ndani na nje ya Tanzania. Huyu ni mama shupavu, jasiri, mpambanaji na mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu, ambaye ameamua kujitoa kutoa mchango wake katika kuendeleza na kulinda ustawi wa taifa la Tanzania.
Tumezoea kusema kwamba ‘nabii hasifiki nyumbani’! Inawezekana ni hivyo kwa mama huyu, ambaye kazi anazozifanya zinaheshimika na kusifiwa kwenye ulingo wa kimataifa kuliko hapa nyumbani? Inawezekana ni kwa vile kazi anayoifanya mama huyu inaigusa serikali jichoni au kwa vile amejifunga kibwebwe kupambana na mfumo dume na kutaka kuutokomeza? Au labda ni kwa vile bado viongozi wengi kwenye ngazi ya maamuzi katika taifa letu ni wanaume?
Juzi, sote tumeshuhudia kwenye vyombo vya habari Dk. Bisimba akisoma taarifa ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kuamua kuiburuza Serikali ya Tanzania kwenye Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) iliyoko The Hague, Uholanzi.
Hiki ni kitendo cha ujasiri na kujitoa, maana ni wachache wanaoweza kuthubutu kufanya hivyo bila kuogopa matokeo yake.
Hata hivyo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, kinachoongozwa na Bisimba, kimekuwa mstari wa mbele kutetea haki za watoto, wanawake na watu wote wanaokandamizwa; kunyang’anywa ardhi yao na matuko mengine ya kifisadi yanayoendelea katika taifa letu. Kituo hiki kimekuwa sauti ya wanyonge.
Mama huyu amejitofautisha na baadhi ya watu wanaoongoza mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) mbalimbali katika taifa letu la Tanzania; hata kama NGO’s hizo zinakuwa ni za kutetea haki za binadamu, viongozi hao wamekuwa wakifanya kazi kwa malengo ya kupata mshahara tu!
Au kwa lengo la kujenga majina yao na kujitafutia sifa. Ni tofauti kabisa na Bisimba, ambaye Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimekuwa sehemu ya maisha yake.
Bila unafiki na kujipendekeza, Bisimba anaonekana wazi kuguswa na kila aina yoyote ile ya ukiukwaji haki za binadamu katika taifa letu. Amekuwa mstari wa mbele kupinga ufisadi, rushwa na uporwaji wa rasilimali katika taifa letu.
Ameshiriki kuipigania demokrasia na utawala bora na kilio cha katiba mpya katika taifa letu. Haogopi kusimama na kusema wazi msimamo wake na msimamo wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.
Yuko tayari kusema hata yale yasiyopendeza kwenye masikio ya watawala.
Mama huyu aliyezaliwa mnamo mwaka wa 1954 mkoani wa Kilimanjaro, ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinacholinda na kutetea haki za binadamu za kila Mtanzania na kuhakikisha kwamba kila raia anakingwa na aina zote za udhalilishaji.
Mapenzi ya kutetea haki za binadamu na moyo wa unaharakati yalionekana kwake kwenye miaka ya 1970 alipokuwa akisoma sekodari ya Korogwe kule Tanga.
Alifukuzwa shule kwa muda, baada ya kukataa shinikizo la walimu wake kuomba msamaha kwa barua ya kudhalilisha aliyoandikiwa mwalimu mkuu wa shule. Alikataa kuomba msamaha wa kosa ambalo yeye hakutenda.
Kwa vile alikuwa msaidizi wa kiranja wa shule alikubali kufukuzwa kuliko kuomba msamaha. Baba yake mzazi alikwenda kumwombea msamaha, lakini walimu walikataa. Hadi alipoamua baadaye kuzungumza na walimu na hatimaye kuomba msamaha kwa kosa ambalo hakulitenda mwenyewe.
Tukio hili lilimjengea moyo wa ujasiri ambao hadi leo hii zaidi ya miaka 40, amekuwa akitetea haki za wanyonge, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee.
Mama huyu, alikuwa kati ya watu wa kwanza kumshughulikia Dk. Stephen Ulimboka alipotekwa, kupigwa na kuteswa.
Kila mtu alishangaa jinsi mama huyu alivyopata habari haraka juu ya tukio hilo la kinyama na kufanya haraka kushiriki kutoa msaada kwa Dk. Ulimboka.
Alimsaidia kumfikisha hospitali na kuendelea kuishinikiza serikali ifanye uchunguzi wa kina kubaini watu waliofanya unyama huo.
Wakati wa mgomo wa madaktari, sauti ya Bisimba ilisikika kote kwenye vyombo vya habari. Yeye na wanaharakati wengine waliishinikiza serikali kufanya haraka kuumaliza ili kunusuru uhai wa raia wasiokuwa na hatia.
Na katika hali isiyokuwa ya kawaida mama huyu na wanaharakati wengine walikamatwa na polisi na kuhojiwa wakati walipofika Muhimbili, kutaka kujua kinachoendelea.
Mwaka 2001, alikuwa mwanamke mwanaharakati wa kwanza kupinga na kulaani mauaji yaliyotokea Zanzibar. Kitendo hicho kilimletea sifa ndani na nje ya Tanzania.
Mwaka 2008 alikuwa mwanamke wa kwanza kupokea tuzo ya Mwanamke Jasiri inayotolewa na Balozi wa Amerika nchini Tanzania.
Mama huyu amekuwa mstari wa mbele kupinga hukumu ya kifo. Siku ya Kupinga Hukumu ya Kifo inaangukia siku yake ya kuzaliwa ambayo ni Oktoba 10, hivyo mwaka huu anapoadhimisha miaka 58 ya kuzaliwa, ana imani kubwa kwamba iko siku adhabu hii ya kifo itakuja kufutwa nchini Tanzania.
Mama huyu ni kati ya watu wanaotamani kuona Tanzania inawaruhusu wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni kuendelea na masomo, na elimu ya kujitambua inafundishwa shuleni.
Kwa maoni yake, wakati mwingine wasichana wanapachikwa mimba kwa kuwa na uelewa mdogo juu ya kujamiana; na kwamba wazazi wasione aibu kuongea na watoto wao juu ya suala la kujitambua na mahusiano, maana ukimya katika hili ni hatari zaidi kuliko faida.
Mama huyu yuko mstari wa mbele kupinga vifo vya wanawake wakati wa kujifungua na vifo vya watoto wadogo. Ameunga mkono na kushiriki kampeni zote zinazoendelea za kupambana kupunguza vifo vya wajawazito.
Pia kwa kupitia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu anaongoza kampeni ya kutokomeza ukeketaji, kuwarithi wajane na aina nyingine ya unyanyasaji kwa wanawake.
Mama huyu alianza kukiongoza Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu mwaka 1996, na ni mmoja wa waanzilishi wa kituo hiki cha kutetea na kulinda haki za binadamu.
Ni mjane tangu mwaka 1994. Ana watoto wanne, wawili ni mainjinia, mmoja ni daktari na mwingine ni mhasibu. Lakini pia anatunza watoto yatima nyumbani kwake na ni mwanachama wa wanawake wajane katika kanisa anapoabudu.
Mbali na kuwatunza watoto yatima nyumbani kwake, yeye amekuwa sauti ya watoto wanaojilea na kujitunza.
Wakati kuna watafiti wanaopinga Tanzania kuwa na familia za watoto wanaojilea wenyewe na kujitunza, Bisimba anaamini kwamba Makete na Karagwe, alikofanyia utafiti wa tasinifu yake ya shahada ya uzamifu, kuna familia za watoto wanaojilea na kujitunza kutokana na janga la ugonjwa wa ukimwi.
Mwaka 2008 mpaka 2001, alichukua likizo ya masomo na kwenda Uingereza kuchukua shahada ya uzamifu kwenye sheria na haki za binadamu.
Tasinifu yake ulikuwa ni utafiti juu ya haki za watoto. Alitaka sauti ya watoto wa Afrika isikike, alitaka kujua jinsi watoto wanavyouelewa mfumo wa serikali. Anaamini kwamba kwa kuelewa mawazo ya watoto, serikali yoyote inaweza kutenda vizuri siku zinazokuja, maana watoto wa leo ndio viongozi wa kesho.
Kabla ya kujiunga na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, mama huyu alikuwa mwalimu wa Kiingereza na Kiswahili katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima alikofanya kazi kwa kipindi cha miaka 10.
Marehemu mume wake ndiye aliyemshauri kusomea sheria. Wakati anajiunga na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, alikuwa bado anafundisha taasisi na kujitolea kwenye Shirika la WILDAF (Women in Law and Development in Africa) ambalo aliliwakilisha kwenye mkutano wa wanawake wa Beijing mwaka 1995.
Mama huyu ni kiongozi wa mfano. Hata wafanyakazi wenzake wanampenda na kumheshimu. Wengi amewaambukiza roho ya kutetea haki za binadamu na ujasiri wa kusimama kidete mbele ya haki.
Ukifika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, unakutana na mkurugenzi ambaye licha ya kuwa kiongozi wa kituo hicho, ni mama mwenye sifa zote za umama; kulea, kuelekeza, kujali, kutokuwa na uroho wa elimu, kuwashughulikia wengine, kuguswa na matatizo ya wengine na kuambukiza roho ya ujasiri kwa wafanyakazi wenzake.
Mama huyu pamoja na kazi kubwa alizonazo za kukiongoza kituo, bado ana nafasi ya kuihudumia familia yake, kuangalia mpira na watoto na wajukuu zake na pia kupata nafasi ya kuimba kwenye kwaya ya kanisa.
Huyo ndiye Bisimba, mwanamke shujaa, jasiri, msomi, mzalendo, mwanaharakati na mtetezi wa haki za binadamu.

Mahakama Kuu yamliza Dk. Slaa






HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali pingamizi lilowasilishwa mbele yake na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, lililokuwa likiomba mahakama hiyo ifute kesi ya madai iliyofunguliwa na Rose Kamili Slaa aliyeomba imzuie mumewe Dk. Slaa asifunge ndoa na mchumba wake, Josephine Mushumbusi.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Laurence Kaduri ambaye alisema baada ya kupitia kwa kina pingamizi lilowasilishwa na Dk. Slaa na majibu yaliyojibiwa na mlalamikaji Rose anayetetewa na wakili wa kujitegemea Joseph Thadayo, ameona hoja za kutaka mahakama iifute kesi ya msingi iliyofunguliwa na Rose ni dhahifu na hivyo amezitupilia mbali.
Jaji Kaduli alisema Dk. Slaa alikosea kudai kuwa Rose hakuwa na haki ya kufungua kesi hiyo ya kumzuia asifunge ndoa na mchumba wake, Josephine, kwa sababu hawakuwahi kufunga ndoa ila kulikuwa na dhana ya ndoa.
“Mahakama hii inaitupilia mbali tena kwa gharama pingamizi hilo la Dk. Slaa linalosema kuwa Rose hakuwa na haki ya kupinga ndoa yake kwa sababu hakuwa mke wake na wala hawajawahi kufunga ndoa kwa sababu sheria ya ndoa inasema mtu ambaye umeishawahi kuishi kama mke na mume kwa zaidi ya miaka miwili, inawahesabu kama ni wana ndoa.
“Hivyo mahakama hii inasema Rose ana haki ya kufungua kesi ya kuzuia ndoa ya wadaiwa, yaani Slaa na Josephine na natupilia mbali pingamizi la Slaa na kwamba kesi ya msingi itakuja kutajwa mahakamani hapa Novemba 6 mwaka huu,” alisema Jaji Kaduri.
Kesi hiyo ya madai ya ndoa ilifunguliwa mahakamani hapo na Rose dhidi ya Dk. Slaa na Josephine kwa mara ya kwanza mapema Julai mwaka huu, akiiomba mahakama isikubali shauri hilo lipelekwe kwenye Bodi ya Maridhiano ya Masuala ya Ndoa kwa ajili ya kupatanishwa.
Dai la pili, Rose anaiomba mahakama itangaze yeye na Dk. Slaa bado ni wanandoa, na dai la tatu anaiomba mahakama itamke kuwa ndoa baina yake na Dk. Slaa bado halali kisheria na kwamba ndoa nyingine itakayofungwa kinyume na sasa itakuwa ni batili. Katika dai lake la nne, mlalamikaji ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), anadai mdaiwa wa pili (Josephine) alimshawishi mumewe kuivuruga ndoa yake.
Pia nia ya wadaiwa hao wawili ya kutaka kufunga ndoa waliyopanga ifungwe Julai 21 mwaka huu katika eneo lolote lile, ndoa hiyo ihesabike kuwa ni batili.
Aidha, anaiomba mahakama iwaamuru wadaiwa wamlipe fidia ya shilingi milioni 50 kama gharama za matunzo ya watoto wawili ambao ni Emiliana Slaa na Linus Slaa aliyezaliwa mwaka 1987 ambao amekuwa akiwahudumia tangu mwaka 2009 baada ya mume wake kumkimbia.
Pia anaiomba mahakama imwamuru mdaiwa wa pili (Josephine) amlipe fidia ya sh mil. 500 kwa sababu alimsababishia usumbufu mkubwa na kumharibia ndoa yake, na kuongeza kwa kuiomba mahakama hiyo impatie nafuu nyingine ambazo itaona inafaa.

Jeshi, FFU wazima maandamano Dar • Zanzibar waharibu hosteli, wang’oa misalaba




JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) jana lililazimika kuingia mtaani katika jitihada za kuzima ghasia kubwa zilizoligeuza eneo zima la Kariakoo jijini Dar es Salaam kuwa uwanja wa mapambano.
Mapambano yalizuka baada ya kundi la wafuasi wa kiongozi wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, waliotaka kuandamana kuelekea Ikulu jijini Dar es Salaam kupinga kukamatwa kwa viongozi wao.
Askari wa JWTZ waliokuwa katika magari matano, wakiwa wamesheheni zana za kivita, waliwasili katika eneo la Kariakoo, na wengine kuelekea Ikulu kudhibiti maandamano ya wafuasi hao.
Rais Jakaya Kikwete aliyewasili Ikulu majira ya saa 7:48 mchana alilakiwa na ulinzi mkali wa askari wa JWTZ, huku mmoja wa wafuasi hao akiwa anashikiliwa na polisi.
Wafuasi hao pia walikuwa na chupa za maji, miswaki na sabuni ndani ya kanzu zao wakionekana kuwa tayari kwa lolote.
Vurugu hizo zilianza majira ya saa 7 mchana katika Mtaa wa Msimbazi jirani na Kituo cha Polisi, mara baada ya Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa katika Msikiti wa Idrisa, ambapo waumini hao waligawiwa vipeperushi vya kuwahimiza kuandamana kuelekea Ikulu.
Wafuasi hao walizidi kuongezeka baada ya kuungana na wenzao waliotoka katika Msikiti wa Kwamtoro na hivyo kufanya mapambano kuwa makali zaidi, huku baadhi ya watu wanaoaminika kuwa wezi na vibaka wakipora bidhaa mbalimbali za wafanyabiashara.
Ghasia hizo zilisababisha kusimama kwa shughuli zote za kijamii, na kulazimika kufungwa kwa barabara zote katika eneo hilo.
Wakati hali ikizidi kuwa tete, ndipo magari matano yaliyokuwa yamebeba askari wa JWTZ wakiwa na silaha za moto yaliwasili katika eneo hilo kwa mbwembwe.
Askari hao walionekana kuwa tayari kwa lolote, lakini hawakuweza kuanza mapambano yoyote wala kutumia silaha kukabiliana na wafuasi hao. Katika vurugu hizo zaidi ya watu 100 wamekamatwa.
Waandamanaji hao walikuwa wamebeba vipeperushi vilivyokuwa na maandishi ya kupinga kukamatwa kwa Waislamu na kuteswa, akina mama kudhalilishwa na kuwekwa ndani, misikiti kupigwa mabomu Mbagala, Polisi kuingia na viatu msikitini na kulaani hatua ya Rais Kikwete kuwapa pole Wakristo katika sakata la vurugu za Mbagala.
Mmoja wa wafuasi waliokamatwa katika eneo la Ikulu aliwaeleza askari waliomkamata kuwa alikuwa tayari kufa na kwenda peponi kwa madai kuwa alikuwa akishiriki vita ya jihadi kwa ajili ya Allah.
Zanzibar hakukaliki
Huko Zanzibar, hali ya usalama iliendelea kutoweka kufuatia kuongezeka kwa ghasia zinazoaminika kufanywa na wafuasi wa kundi la Uamsho.
Wafuasi wa kundi hilo juzi usiku walivamia makaburi ya Wakristo na kuyaharibu ikiwa ni pamoja na kubomoa misalaba, huku wakitishia kuchoma moto Kanisa la Anglikana.
Watu hao pia waliharibu hosteli inayomilikiwa na Kanisa la Anglikana Mkunazini, huku wakitishia kufanya uharibifu zaidi.
Kutokana na hali kuwa tete zaidi, baadhi ya wakazi wa Unguja ambao ni Wakristo wameanza kuukimbia mji huo, ambapo jana zaidi ya watu 60 waliwasili katika bandari ya Dar es Salaam.
Kuchafuka kwa hali hiyo kumeiweka Serikali ya Umoja wa Kitaifa katika wakati mgumu hasa kufuatia hatua ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka CCM kususia vikao vyake juzi wakipinga ghasia hizo na kuwataka wakuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Bara na Zanzibar kujiuzulu.
Mihadhara yapigwa marufuku
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiki, amepiga marufuku mihadhara yote ya dini mpaka hali ya usalama itakaporejea.
Alizungumza hayo jana katika mkutano uliowajumuisha Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC), Padri Anthony Makunde na kuzitaka mamlaka zote zinazoshughulika na utoaji vibali vya mihadhara hiyo kuacha kufanya hivyo.
Naye Padre Makunde alitoa rai kwa Watanzania kuendelea kuvumilia na kudumisha upendo na mshikamano uliopo miaka mingi baina yao na kusema kuwa njia pekee ya kufikia suluhu ni mazungumzo bila jazba na hasira.
Kwa upande wake Sheikh Alhad aliwataka Waislamu, maimamu na masheikh kuwa na subira na kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani na kutojidanganya kuwa na jihad kwani haiji kwa uvunjifu wa sheria na kwamba nidhamu ya dini hiyo na utaratibu wake unakataa vitendo hivyo.
Lwaitama aishukia serikali
Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Azavel Lwaitama, amesema udhaifu wa serikali ndio umefanya suala la vurugu za wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Kiislamu kulifikisha taifa hapa lilipo.
Udhaifu huo Lwaitama alisema ulianza tangu katika kipindi cha fujo za Mwembechai ambapo serikali haijaonesha jitihada zozote za kulitafutia suala hilo ufumbuzi.
Kutokana na hali hiyo, Lwaitama alitaka busara itumike zaidi katika kutatua fujo zinazoendelea sasa hivi badala ya kutumia nguvu kwani inaweza kuifikisha nchi pahali pasipotarajiwa.
Alisema kitendo cha kukamatwa kwa Sheikh Ponda sasa hivi na kusomewa mashitaka ya matukio yaliyotendeka tangu huko nyuma baada tu ya kuvamia kiwanja ni kama kutaka kuficha kitu nyuma ya pazia.
“Mimi naishangaa sana hii serikali kwani wakati matukio yale ya nyuma yalipotokea walikuwa wanashindwa nini kumkamata Sheikh huyo? Hebu katika hili busara zaidi itumike kwani na yeye ana wafuasi wake wengi hivyo watakapoamua kuingia barabarani hakuna atakayesalimika,” alisema.
Pia hakusita kuwapongeza viongozi wa madhehebu ya Kikristu kwa hatua yao walioichukua ya kuwa wavumilivu katika kipindi hiki na kukazana na maombi.
Kuhusu mtoto aliyekojolea msaafu, Lwaitama alisema hayo yote yametokana na matukio ya mfumo wa elimu uliopo sasa hivi hapa nchini wa kutoheshimu dini za wenzao.
Alisema umri wa mtoto huyo wa miaka 14 sio mdogo kihivyo kiasi cha kushindwa kutambua kile alichokuwa anakifanya ni kosa na badala yake alisema elimu wanayopewa watoto siku hizi haiwajengi katika kuweza kuishi na watu tofauti kwenye jamii.
Kova akanusha
Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi, Suleiman Kova amekanusha taarifa iliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Jeshi la Polisi limewataka Waislamu wote wa kikundi hicho kujisalimisha kwa jeshi hilo.
Kova alisema kuwa watu wanaotakiwa kujisalimisha ni sita na kuwataja kuwa ni Mukadam Saleh Kondo, Saleh Juma Bungo, Shaaban Mapeo, Jaafar Mneki, Rajab Katimba na Amani Moshi.
Hadi tunakwenda mitamboni, hali katika mitaa mingi ya Kariakoo ilikuwa haijatulia na kulikuwa na wasiwasi kwamba, watu hao walikuwa wakijikusanya kuendeleza mapambano na polisi.

Ikulu yamkana aliyemtesa Ulimboka






WAKATI sakata la kutekwa, kuteswa na kisha kutupwa katika msitu wa Mwabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar ss Salaam kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk Steven Ulimboka, likiwa limefikia miezi mitatu, Ikulu imeibuka na kumkana mtumishi wake Ramadhan Ighondu anayetajwa kuhusika katika unyama huo.
Mwanzoni mwa wiki Dk. Ulimboka alitoa tamko akisema kwamba Ighondu ndiye aliyehusika na sakata la kumteka na kumtesa vibaya katika jaribio la kutaka kumuua.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumamosi, Ikulu jana, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, alisema kuwa hamfahamu mtumishi huyo aliyetajwa na Ulimboka.
Alisisitiza kuwa Ikulu haipo kwa ajili ya kuteka na kutesa watu, hivyo wale wanaodai kuwa mtumishi wa ofisi hiyo anahusika na tukio hilo wanaongea tu.
“Wala simfahamu…Ikulu haipo kwa ajili ya kutesa watu na hao wanaomtaja mtumishi huyo kuwa yupo Ikulu hao wanazungumza tu,” alisema.
Wakati Balozi Sefue akitoa kauli hiyo, juzi Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alisisitiza kuwa Ikulu haihusiki na kwamba Rais Jakaya Kikwete alishalijibu suala hilo.
Katika tamko lake la kiapo lililotolewa kwa waandishi wa habari, Dk. Ulimboka, kupitia kwa wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheere, alisema anamfahamu mtesaji wake, na kwamba hata akikamatwa leo hii, atakwenda kufanya utambuzi.
Alisema anashangaa kwamba polisi wameshindwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, licha ya kwamba alishatajwa na gazeti la MwanaHALISI na katika mtandao wa YouTube.
Alisema: “Nathibitisha kwamba Ramadhan Ighondu alitambulishwa kwetu kwa jina la Abeid. Binafsi ninamfahamu sana bwana huyu kwa sababu alikuwa akitumwa mara kwa mara kuja kukutana na mimi na tumekutana mara kadhaa kabla ya tukio lile.
“Nathibitisha kwamba mfanyakazi huyu wa Ikulu, ndiye aliyenipigia simu na kuniita kwenye kikao ambacho muda mfupi baadaye nilitekwa. Katika mawasiliano hayo, Abeid alikuwa anatumia simu namba 0713 760473.”
Dk. Ulimboka aliongeza kuwa, anakumbuka kuwa Abeid alitambulishwa kwake na kigogo mmoja, akiwa na wawakilishi wengine wa madaktari, kuwa ndiye angehusika katika kuchukua madai na hoja za madaktari katika mgogoro kati yao na serikali.
Kauli ya jana ya Balozi Sefue ni ya tatu kutolewa na Ikulu kuhusu Dk. Ulimboka.
Mara ya kwanza, ilitolewa na Rais Jakaya Kikwete alipokutana na baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ambapo alisema, “Dk. Ulimboka ana nini mpaka Ikulu imteke? Tumteke ili iweje?”
Kikwete alikwenda mbali zaidi na kusema hata Dk. Ulimboka mwenyewe alipokwenda Ikulu akiwa na viongozi wenzake, alinyamaza kimya tu na kwamba waliokuwa wakizungumza ni wengine.
Hata hivyo, kwa kuwa Ikulu imesema haihusiki, na Dk. Ulimboka mwenyewe ametamka kwamba anamjua aliyemtesa, na kwamba anafanya kazi Ikulu, ni juu ya umma kuamua nani anasema ukweli.
Juni 26, mwaka huu, Dk. Ulimboka alitekwa, akapigwa, akang’olewa kucha kabla ya kuokotwa msitu wa Mabwepande na kupelekwa katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) kwa matibabu.
Hata hivyo, baadaye alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi na alirejea nchini Agosti 12, mwaka huu.

Monday, October 15, 2012

The Satanic Verses

From Wikipedia, the free encyclopedia
Jump to: navigation, search
The Satanic Verses
1988 Salman Rushdie The Satanic Verses.jpg
First edition cover
Author(s) Salman Rushdie
Country United Kingdom
Language English
Genre(s) Magic Realism, Novel
Publisher Viking Press
Publication date 1988
Media type Print (Hardback and paperback)
Pages 547 pp
ISBN 0-670-82537-9
OCLC Number 18558869
Dewey Decimal 823/.914
LC Classification PR6068.U757 S27 1988
Preceded by Shame
Followed by Haroun and the Sea of Stories
The Satanic Verses is Salman Rushdie's fourth novel, first published in 1988 and inspired in part by the life of Muhammad. As with his previous books, Rushdie used magical realism and relied on contemporary events and people to create his characters. The title refers to the so-called "satanic verses", a group of alleged Quranic verses that allow intercessory prayers to be made to three Pagan Meccan goddesses: Allāt, Uzza, and Manāt.[1] The part of the story that deals with the "satanic verses" was based on accounts from the historians al-Waqidi and al-Tabari.[1]
In the United Kingdom, the book received positive reviews. It was a 1988 Booker Prize Finalist (losing to Peter Carey's Oscar and Lucinda) and won the 1988 Whitbread Award for novel of the year.[2] The Satanic Verses sparked a major controversy when conservative Muslims accused it of blasphemy and mocking their faith. The outrage among some Muslims resulted in a fatwā calling for Rushdie's death issued by Ayatollah Ruhollah Khomeini, the Supreme Leader of Iran, on 14 February 1989. Although Rushdie himself has never been attacked as a result of the book's creation, Islamic extremists have attacked several connected individuals such as translator Hitoshi Igarashi (leading to, in Igarashi's case, death).

[edit] Plot

The Satanic Verses consists of a frame narrative, using elements of magical realism, interlaced with a series of sub-plots that are narrated as dream visions experienced by one of the protagonists. The frame narrative, like many other stories by Rushdie, involves Indian expatriates in contemporary England. The two protagonists, Gibreel Farishta and Saladin Chamcha, are both actors of Indian Muslim background. Farishta is a Bollywood superstar who specializes in playing Hindu deities. (The character is partly based on Indian film stars Amitabh Bachchan and Rama Rao.[3]) Chamcha is an emigrant who has broken with his Indian identity and works as a voiceover artist in England.
At the beginning of the novel, both are trapped in a hijacked plane flying from India to Britain. The plane explodes over the English Channel, but the two are magically saved. In a miraculous transformation, Farishta takes on the personality of the archangel Gibreel, and Chamcha that of a devil. Chamcha is arrested and passes through an ordeal of police abuse as a suspected illegal immigrant. Farishta's transformation can partly be read on a realistic level as the symptom of the protagonist's developing schizophrenia.
Both characters struggle to piece their lives back together. Farishta seeks and finds his lost love, the English mountaineer Allie Cone, but their relationship is overshadowed by his mental illness. Chamcha, having miraculously regained his human shape, wants to take revenge on Farishta for having forsaken him after their common fall from the hijacked plane. He does so by fostering Farishta's pathological jealousy and thus destroying his relationship with Allie. In another moment of crisis, Farishta realizes what Chamcha has done, but forgives him and even saves his life.
Both return to India. Farishta kills Allie in another outbreak of jealousy and then commits suicide. Chamcha, who has found not only forgiveness from Farishta but also reconciliation with his estranged father and his own Indian identity, decides to remain in India.

[edit] Dream sequences

Embedded in this story is a series of half-magic dream vision narratives, ascribed to the mind of Gibreel Farishta. They are linked together by many thematic details as well as by the common motifs of divine revelation, religious faith and fanaticism, and doubt.
One of these sequences contains most of the elements that have been criticized as offensive to Muslims. It is a transformed re-narration of the life of Muhammad (called "Mahound" or "the Messenger" in the novel) in Mecca ("Jahilia"). At its centre is the episode of the so-called satanic verses, in which the prophet first proclaims a revelation in favour of the old polytheistic deities, but later renounces this as an error induced by Shaitan. There are also two opponents of the "Messenger": a demonic heathen priestess, Hind, and an irreverent skeptic and satirical poet, Baal. When the prophet returns to the city in triumph, Baal goes into hiding in an underground brothel, where the prostitutes assume the identities of the prophet's wives. Also, one of the prophet's companions claims that he, doubting the "Messenger"'s authenticity, has subtly altered portions of the Quran as they were dictated to him.
The second sequence tells the story of Ayesha, an Indian peasant girl who claims to be receiving revelations from the Archangel Gibreel. She entices all her village community to embark on a foot pilgrimage to Mecca, claiming that they will be able to walk across the Arabian Sea. The pilgrimage ends in a catastrophic climax as the believers all walk into the water and disappear, amid disturbingly conflicting testimonies from observers about whether they just drowned or were in fact miraculously able to cross the sea.
A third dream sequence presents the figure of a fanatic expatriate religious leader, the "Imam," in a late-20th-century setting. This figure is a transparent allusion to the life of Ayatollah Khomeini in his Parisian exile, but it is also linked through various recurrent narrative motifs to the figure of the "Messenger".

[edit] Literary criticism and analysis

Overall, the book received favourable reviews from literary critics. In a 2003 volume of criticism of Rushdie's career, influential critic Harold Bloom named The Satanic Verses "Rushdie's largest aesthetic achievement".[4]
Timothy Brennan called the work "the most ambitious novel yet published to deal with the immigrant experience in Britain" that captures the immigrants' dream-like disorientation and their process of "union-by-hybridization". The book is seen as "fundamentally a study in alienation."[2]
Muhammd Mashuq ibn Ally wrote that "The Satanic Verses is about identity, alienation, rootlessness, brutality, compromise, and conformity. These concepts confront all migrants, disillusioned with both cultures: the one they are in and the one they join. Yet knowing they cannot live a life of anonymity, they mediate between them both. The Satanic Verses is a reflection of the author’s dilemmas." The work is an "albeit surreal, record of its own author's continuing identity crisis."[2] Ally said that the book reveals the author ultimately as "the victim of nineteenth-century British colonialism."[2] Rushdie himself spoke confirming this interpretation of his book, saying that it was not about Islam, "but about migration, metamorphosis, divided selves, love, death, London and Bombay."[2] He has also said "It’s a novel which happened to contain a castigation of Western materialism. The tone is comic."[2]
After the Satanic Verses controversy developed, some scholars familiar with the book and the whole of Rushdie's work, like M. D. Fletcher, saw the reaction as ironic. Fletcher wrote "It is perhaps a relevant irony that some of the major expressions of hostility toward Rushdie came from those about whom and (in some sense) for whom he wrote."[5] He said the manifestations of the controversy in Britain "embodied an anger arising in part from the frustrations of the migrant experience and generally reflected failures of multicultural integration, both significant Rushdie themes. Clearly, Rushdie's interests centrally include explorations of how migration heightens one's awareness that perceptions of reality are relative and fragile, and of the nature of religious faith and revelation, not to mention the political manipulation of religion. Rushdie's own assumptions about the importance of literature parallel in the literal value accorded the written word in Islamic tradition to some degree. But Rushdie seems to have assumed that diverse communities and cultures share some degree of common moral ground on the basis of which dialogue can be pieced together, and it is perhaps for this reason that he underestimated the implacable nature of the hostility evoked by The Satanic Verses, even though a major theme of that novel is the dangerous nature of closed, absolutist belief systems."[5]
Rushdie's influences have long been a point of interest to scholars examining his work. According to W. J. Weatherby, influences on The Satanic Verses were listed as Joyce, Italo Calvino, Kafka, Frank Herbert, Pynchon, Mervyn Peake, Gabriel Garcia Marquez, Jean-Luc Godard, J. G. Ballard, and William Burroughs.[6] Chandrabhanu Pattanayak notes the influence of William Blake's The Marriage of Heaven and Hell and Mikhail Bulgakov's The Master and Margarita (influences Rushdie admitted to).[5] M. Keith Booker likens the book to James Joyce's Finnegans Wake.[5] Al-'Azm notes the influence of François Rabelais' works.[5] Others have noted an influence of Indian classics such as the Mahabharata and the Arabic Arabian Nights.[5] Angela Carter writes that the novel contains "inventions such as the city of Jahilia, 'built entirely of sand,' that gives a nod to Calvino and a wink to Frank Herbert".[7]
Srinivas Aravamudan’s analysis of The Satanic Verses was perceived by other scholars as hailing the book as a proof "demonstrating the compatibility of postmodernism and post-colonialism in the one novel."[5] Aravamudan himself stressed the satiric nature of the work and held that while it and Midnight's Children may appear to be more "comic epic", "clearly those works are highly satirical" in a similar vein of postmodern satire pioneered by Joseph Heller in Catch-22.[5]
The Satanic Verses continued to exhibit Rushdie's penchant for organizing his work in terms of parallel stories. Within the book "there are major parallel stories, alternating dream and reality sequences, tied together by the recurring names of the characters in each; this provides intertexts within each novel which comment on the other stories."[5] The Satanic Verses also exhibits Rushdie's common practice of using allusions in order to invoke connotative links. Within the book he referenced everything from mythology to "one-liners invoking recent popular culture" sometimes using several per page.[5] Chapter VII was especially noted by for such usage.[5]

[edit] Controversy

The novel caused great controversy in the Muslim community for what some Muslims believed were blasphemous references. Rushdie was accused of mis-using freedom of speech.[8] As the controversy spread, the import of the book was banned[9] in India and it was burned in demonstrations in the United Kingdom. In mid-February 1989, following a violent riot against the book in Pakistan, the Ayatollah Ruhollah Khomeini, Supreme Leader of Iran and a Shi'a Muslim scholar, issued a fatwa calling on all good Muslims to kill Rushdie and his publishers, or to point him out to those who can kill him if they cannot themselves.[10] Although the British Conservative government under Margaret Thatcher gave Rushdie round-the-clock police protection, many politicians on both sides were hostile to the author. British Labour MP Keith Vaz led a march through Leicester shortly after he was elected in 1989 calling for the book to be banned, while Conservative MP Norman Tebbit, the party's former chairman, called Rushdie an "outstanding villain" whose "public life has been a record of despicable acts of betrayal of his upbringing, religion, adopted home and nationality".[11] Meanwhile the Commission for Racial Equality and a liberal think tank, the Policy Studies Institute held seminars on the Rushdie affair. They did not invite the author Fay Weldon who spoke out against burning books, but did invite Shabbir Akhtar, a Cambridge philosophy graduate who called for "a negotiated compromise" which "would protect Muslim sensibilities against gratuitous provocation". The journalist and author Andy McSmith wrote at the time "We are witnessing, I fear, the birth of a new and dangerously illiberal "liberal" orthodoxy designed to accommodate Dr Akhtar and his fundamentalist friends."[12]
Following the fatwa, Rushdie was put under police protection by the British government. Despite a conciliatory statement by Iran in 1998, and Rushdie's declaration that he would stop living in hiding, the Iranian state news agency reported in 2006 that the fatwa would remain in place permanently since fatwas can only be rescinded by the person who first issued them, and Khomeini had since died.[13]
Rushdie has never been physically harmed for the book, but others associated with it have suffered violent attacks. Hitoshi Igarashi, its Japanese translator, was stabbed to death on 11 July 1991. Ettore Capriolo, the Italian translator, was seriously injured in a stabbing the same month.[14] William Nygaard, the publisher in Norway, was shot three times in an attempted assassination in Oslo in October 1993, but survived. Aziz Nesin, the Turkish translator, was the intended target in the events that led to the Sivas massacre on 2 July 1993 in Sivas, Turkey, which resulted in the deaths of 37 people.[15] Individual purchasers of the book have not been harmed. The only nation with a predominantly Muslim population where the novel remains legal is Turkey.[citation needed]
In September 2012, Rushdie expressed doubt that The Satanic Verses would be published today because of a climate of "fear and nervousness".[16]