Saturday, October 20, 2012

MAONI YA FRANK LUPEKE

KANUNI KUMI ZA KUIKOMBOA TANZANIA KUTOKA KWA WAKOLONI WEUSI (CCM)
1. Usiwe msaliti kwa NCHI yako. kuwa MZALENDO
2. Usiwe MVIVU wa kufikiri. Kuwa MDADISI.
3. Usiwe Mwoga, WOGA WAKO NDIYO UMASKINI WAKO.
4. Toa maoni tupate KATIBA bora. Na hakikisha unajiandikisha kwenye DAFTARI LA WAPIGA KURA.
5. Usitoe wala Kupokea RUSHWA. RUSHWA NI ADUI WA HAKI.
6. Usiwe MROHO wa MADARAKA kama LOWASA na CUF.
7. Tambua WAJIBU na HAKI zako. Hasa ya KUPIGA KURA.
8. Usiwasikilize WAGOMBEA na VIONGOZI wa CCM, Maana WATAKULAGHAI.
9. Usiwe na TAMAA ya vitu kama KANGA, KOFIA, TSHERT, VILEMBA na UBWABWA wa CCM.
10. (Amri Kuu)
Usimpigie KURA mgombea Yeyote wa CCM katika UCHAGUZI wowote ule kuanzia MWENYEKITI wa KIJIJI/MTAA, DIWANI, MBUNGE na RAIS.

MUNGU WAFUNGUE WATANZNIA, MUNGU IBARIKI TANZANIA

‘Maoni ya wananchi ni muhimu katiba mpya’





MWENYEKITI wa Mtandao wa Asasi za Kiraia Mkoa Lindi (LANGO), Mudhihiri Mewile, amewataka wakazi wa Somanga kutumia fursa zilizopo za kutoa maoni ya katiba ili nchi ipate katiba yenye kujali maslahi ya taifa na si ya wanasiasa.
Akizungumza kwenye mdahalo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya katiba uliofanyika jana kwenye Jimbo la Kilwa Kaskazini, Mawile aliwataka wananchi kutoogopa kutoa maoni katika katiba mpya, kwani ni mali yao.
Katika mdahalo huo uliofanyika katika maeneo ya Kijiji cha Somanga, wananchi wengi walijitokeza kutoa maoni ambapo Ally Mohamedi alitaka katiba ijayo iangalie masilahi ya wazee kwani ndio waliochangia mapato ya nchi hii.
Husna Seleman alitaka suala la elimu ya vitendo mashuleni kuanzia shule ya msingi mpaka vyuoni lidhibitiwe na isiwe inafanyiwa mabadiliko ya mitaala mara kwa mara.
“Kwa upande wangu nilitaka suala la elimu kwa vitendo lianzie katika shule za msingi hadi vyuoni kwani itasaidia sana, itakapotokea mwanafunzi ameshindwa mitihani yake ataweza kujiajiri mwenyewe,” alisema Husna.

Ulimboka amefungua milango ya uchunguzi




VYOMBO vingi vya habari juzi vimetawaliwa na habari inayomhusu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka, ambaye ameweka bayana kile kilichomsibu usiku wa Juni 26 mwaka huu, katika msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Dk. Ulimboka ameeleza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwataja kwa majina baadhi ya watendaji wa Ikulu ambao anaamini kuwa walihusika kwa namna moja ama nyingine katika tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwake.
Tunampongeza Dk. Ulimboka kwa kuweka bayana kile anachokiamini kuwa ndiyo ukweli wa tukio la kutekwa kwake, kwani tunadhani sasa atakuwa amefungua milango ya sakata hilo kuchunguzwa kwa umakini kukata mzizi wa fitina.
Ni kweli kesi ya tukio hilo imefunguliwa mahakamani ambapo raia mmoja wa Kenya anashtakiwa kufanya tukio hilo, lakini bado haizuii uchunguzi wa kina kuendelea hasa wakati huu ambapo muhusika amejitokeza wazi kutoa ushirikiano wa kuwatambua wale waliomfanyia kitendo hicho.
Tume ya uchunguzi iliyoundwa na Jeshi la Polisi kuchunguza tukio hio, imekuwa ikinyooshewa kidole na baadhi ya wadau wakiwemo madaktari wenyewe kwa madai kuwa haiko huru kwani baadhi ya wajumbe wake ni watuhumiwa.
Hata Dk. Ulimboka katika taarifa yake hiyo ya jana, amesisitiza kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano wa kina endapo kitaundwa chombo huru kuchunguza tukio hilo.
Ni vyema serikali ikajitafakari upya ili kuondoa sintofahamu hii vinywani mwa watu kwa kuunda chombo huru ili kuchunguza sakata hilo na hivyo kumfanya Dk. Ulimboka na Watanzania wengine kujiona wana haki ya kuishi kwa amani katika nchi yao.
Dk. Ulimboka ameeleza wazi kuwa anathibitisha kwamba Ramadhani Ighondu alitambulishwa kwao kwa jina la Abeid. Kwamba Binafsi anamfahamu sana bwana huyu kwa sababu alikuwa akitumwa mara kwa mara kuja kukutana naye na wamekutana mara kadhaa kabla ya tukio lile.
Alisema wazi kuwa anakumbuka kuwa Abeid alitambulishwa kwao na kigogo mmoja, akiwa pamoja na wawakilishi wengine wa madaktari kuwa yeye (Ramadhani Ighondu) ndiye atakayehusika katika kuchukua madai na hoja za madaktari katika mgogoro kati ya madaktari na serikali.
Kwamba anathibitisha kwamba mfanyakazi huyu wa Ikulu, ndiye aliyempigia simu na kumuita kwenye kikao ambako muda mfupi baadaye alitekwa. Katika mawasiliano hayo, Abeid alikuwa anatumia simu namba 0713 760473.
Dk. Ulimboka amebainisha kwamba hakuna shaka kwamba anamtambua Abeid kwa sura na namba aliyokuwa anatumia kuwasiliana naye mpaka siku ya kutekwa kwake.
Hivyo, kwa maelezo hayo ya Dk. Ulimboka, hatuhitaji kuibua mijadala ya malumbano ya nani kafanya nini na nani hakuhusika, isipokuwa jambo la msingi hapa ni kuundwa chombo huru kitakachokuja na majibu ya kumaliza utata huu, ndiyo maana tunasema Dk. Ulimboka amefungua milango ya uchunguzi.

DK. HELEN BISIMBA: Mwanaharakati mtetezi wa haki za binadamu




HELEN Kijo Bisimba, ni jina linalosikika ndani na nje ya Tanzania. Huyu ni mama shupavu, jasiri, mpambanaji na mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu, ambaye ameamua kujitoa kutoa mchango wake katika kuendeleza na kulinda ustawi wa taifa la Tanzania.
Tumezoea kusema kwamba ‘nabii hasifiki nyumbani’! Inawezekana ni hivyo kwa mama huyu, ambaye kazi anazozifanya zinaheshimika na kusifiwa kwenye ulingo wa kimataifa kuliko hapa nyumbani? Inawezekana ni kwa vile kazi anayoifanya mama huyu inaigusa serikali jichoni au kwa vile amejifunga kibwebwe kupambana na mfumo dume na kutaka kuutokomeza? Au labda ni kwa vile bado viongozi wengi kwenye ngazi ya maamuzi katika taifa letu ni wanaume?
Juzi, sote tumeshuhudia kwenye vyombo vya habari Dk. Bisimba akisoma taarifa ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kuamua kuiburuza Serikali ya Tanzania kwenye Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) iliyoko The Hague, Uholanzi.
Hiki ni kitendo cha ujasiri na kujitoa, maana ni wachache wanaoweza kuthubutu kufanya hivyo bila kuogopa matokeo yake.
Hata hivyo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, kinachoongozwa na Bisimba, kimekuwa mstari wa mbele kutetea haki za watoto, wanawake na watu wote wanaokandamizwa; kunyang’anywa ardhi yao na matuko mengine ya kifisadi yanayoendelea katika taifa letu. Kituo hiki kimekuwa sauti ya wanyonge.
Mama huyu amejitofautisha na baadhi ya watu wanaoongoza mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) mbalimbali katika taifa letu la Tanzania; hata kama NGO’s hizo zinakuwa ni za kutetea haki za binadamu, viongozi hao wamekuwa wakifanya kazi kwa malengo ya kupata mshahara tu!
Au kwa lengo la kujenga majina yao na kujitafutia sifa. Ni tofauti kabisa na Bisimba, ambaye Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimekuwa sehemu ya maisha yake.
Bila unafiki na kujipendekeza, Bisimba anaonekana wazi kuguswa na kila aina yoyote ile ya ukiukwaji haki za binadamu katika taifa letu. Amekuwa mstari wa mbele kupinga ufisadi, rushwa na uporwaji wa rasilimali katika taifa letu.
Ameshiriki kuipigania demokrasia na utawala bora na kilio cha katiba mpya katika taifa letu. Haogopi kusimama na kusema wazi msimamo wake na msimamo wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.
Yuko tayari kusema hata yale yasiyopendeza kwenye masikio ya watawala.
Mama huyu aliyezaliwa mnamo mwaka wa 1954 mkoani wa Kilimanjaro, ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinacholinda na kutetea haki za binadamu za kila Mtanzania na kuhakikisha kwamba kila raia anakingwa na aina zote za udhalilishaji.
Mapenzi ya kutetea haki za binadamu na moyo wa unaharakati yalionekana kwake kwenye miaka ya 1970 alipokuwa akisoma sekodari ya Korogwe kule Tanga.
Alifukuzwa shule kwa muda, baada ya kukataa shinikizo la walimu wake kuomba msamaha kwa barua ya kudhalilisha aliyoandikiwa mwalimu mkuu wa shule. Alikataa kuomba msamaha wa kosa ambalo yeye hakutenda.
Kwa vile alikuwa msaidizi wa kiranja wa shule alikubali kufukuzwa kuliko kuomba msamaha. Baba yake mzazi alikwenda kumwombea msamaha, lakini walimu walikataa. Hadi alipoamua baadaye kuzungumza na walimu na hatimaye kuomba msamaha kwa kosa ambalo hakulitenda mwenyewe.
Tukio hili lilimjengea moyo wa ujasiri ambao hadi leo hii zaidi ya miaka 40, amekuwa akitetea haki za wanyonge, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee.
Mama huyu, alikuwa kati ya watu wa kwanza kumshughulikia Dk. Stephen Ulimboka alipotekwa, kupigwa na kuteswa.
Kila mtu alishangaa jinsi mama huyu alivyopata habari haraka juu ya tukio hilo la kinyama na kufanya haraka kushiriki kutoa msaada kwa Dk. Ulimboka.
Alimsaidia kumfikisha hospitali na kuendelea kuishinikiza serikali ifanye uchunguzi wa kina kubaini watu waliofanya unyama huo.
Wakati wa mgomo wa madaktari, sauti ya Bisimba ilisikika kote kwenye vyombo vya habari. Yeye na wanaharakati wengine waliishinikiza serikali kufanya haraka kuumaliza ili kunusuru uhai wa raia wasiokuwa na hatia.
Na katika hali isiyokuwa ya kawaida mama huyu na wanaharakati wengine walikamatwa na polisi na kuhojiwa wakati walipofika Muhimbili, kutaka kujua kinachoendelea.
Mwaka 2001, alikuwa mwanamke mwanaharakati wa kwanza kupinga na kulaani mauaji yaliyotokea Zanzibar. Kitendo hicho kilimletea sifa ndani na nje ya Tanzania.
Mwaka 2008 alikuwa mwanamke wa kwanza kupokea tuzo ya Mwanamke Jasiri inayotolewa na Balozi wa Amerika nchini Tanzania.
Mama huyu amekuwa mstari wa mbele kupinga hukumu ya kifo. Siku ya Kupinga Hukumu ya Kifo inaangukia siku yake ya kuzaliwa ambayo ni Oktoba 10, hivyo mwaka huu anapoadhimisha miaka 58 ya kuzaliwa, ana imani kubwa kwamba iko siku adhabu hii ya kifo itakuja kufutwa nchini Tanzania.
Mama huyu ni kati ya watu wanaotamani kuona Tanzania inawaruhusu wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni kuendelea na masomo, na elimu ya kujitambua inafundishwa shuleni.
Kwa maoni yake, wakati mwingine wasichana wanapachikwa mimba kwa kuwa na uelewa mdogo juu ya kujamiana; na kwamba wazazi wasione aibu kuongea na watoto wao juu ya suala la kujitambua na mahusiano, maana ukimya katika hili ni hatari zaidi kuliko faida.
Mama huyu yuko mstari wa mbele kupinga vifo vya wanawake wakati wa kujifungua na vifo vya watoto wadogo. Ameunga mkono na kushiriki kampeni zote zinazoendelea za kupambana kupunguza vifo vya wajawazito.
Pia kwa kupitia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu anaongoza kampeni ya kutokomeza ukeketaji, kuwarithi wajane na aina nyingine ya unyanyasaji kwa wanawake.
Mama huyu alianza kukiongoza Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu mwaka 1996, na ni mmoja wa waanzilishi wa kituo hiki cha kutetea na kulinda haki za binadamu.
Ni mjane tangu mwaka 1994. Ana watoto wanne, wawili ni mainjinia, mmoja ni daktari na mwingine ni mhasibu. Lakini pia anatunza watoto yatima nyumbani kwake na ni mwanachama wa wanawake wajane katika kanisa anapoabudu.
Mbali na kuwatunza watoto yatima nyumbani kwake, yeye amekuwa sauti ya watoto wanaojilea na kujitunza.
Wakati kuna watafiti wanaopinga Tanzania kuwa na familia za watoto wanaojilea wenyewe na kujitunza, Bisimba anaamini kwamba Makete na Karagwe, alikofanyia utafiti wa tasinifu yake ya shahada ya uzamifu, kuna familia za watoto wanaojilea na kujitunza kutokana na janga la ugonjwa wa ukimwi.
Mwaka 2008 mpaka 2001, alichukua likizo ya masomo na kwenda Uingereza kuchukua shahada ya uzamifu kwenye sheria na haki za binadamu.
Tasinifu yake ulikuwa ni utafiti juu ya haki za watoto. Alitaka sauti ya watoto wa Afrika isikike, alitaka kujua jinsi watoto wanavyouelewa mfumo wa serikali. Anaamini kwamba kwa kuelewa mawazo ya watoto, serikali yoyote inaweza kutenda vizuri siku zinazokuja, maana watoto wa leo ndio viongozi wa kesho.
Kabla ya kujiunga na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, mama huyu alikuwa mwalimu wa Kiingereza na Kiswahili katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima alikofanya kazi kwa kipindi cha miaka 10.
Marehemu mume wake ndiye aliyemshauri kusomea sheria. Wakati anajiunga na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, alikuwa bado anafundisha taasisi na kujitolea kwenye Shirika la WILDAF (Women in Law and Development in Africa) ambalo aliliwakilisha kwenye mkutano wa wanawake wa Beijing mwaka 1995.
Mama huyu ni kiongozi wa mfano. Hata wafanyakazi wenzake wanampenda na kumheshimu. Wengi amewaambukiza roho ya kutetea haki za binadamu na ujasiri wa kusimama kidete mbele ya haki.
Ukifika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, unakutana na mkurugenzi ambaye licha ya kuwa kiongozi wa kituo hicho, ni mama mwenye sifa zote za umama; kulea, kuelekeza, kujali, kutokuwa na uroho wa elimu, kuwashughulikia wengine, kuguswa na matatizo ya wengine na kuambukiza roho ya ujasiri kwa wafanyakazi wenzake.
Mama huyu pamoja na kazi kubwa alizonazo za kukiongoza kituo, bado ana nafasi ya kuihudumia familia yake, kuangalia mpira na watoto na wajukuu zake na pia kupata nafasi ya kuimba kwenye kwaya ya kanisa.
Huyo ndiye Bisimba, mwanamke shujaa, jasiri, msomi, mzalendo, mwanaharakati na mtetezi wa haki za binadamu.

Mahakama Kuu yamliza Dk. Slaa






HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali pingamizi lilowasilishwa mbele yake na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, lililokuwa likiomba mahakama hiyo ifute kesi ya madai iliyofunguliwa na Rose Kamili Slaa aliyeomba imzuie mumewe Dk. Slaa asifunge ndoa na mchumba wake, Josephine Mushumbusi.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Laurence Kaduri ambaye alisema baada ya kupitia kwa kina pingamizi lilowasilishwa na Dk. Slaa na majibu yaliyojibiwa na mlalamikaji Rose anayetetewa na wakili wa kujitegemea Joseph Thadayo, ameona hoja za kutaka mahakama iifute kesi ya msingi iliyofunguliwa na Rose ni dhahifu na hivyo amezitupilia mbali.
Jaji Kaduli alisema Dk. Slaa alikosea kudai kuwa Rose hakuwa na haki ya kufungua kesi hiyo ya kumzuia asifunge ndoa na mchumba wake, Josephine, kwa sababu hawakuwahi kufunga ndoa ila kulikuwa na dhana ya ndoa.
“Mahakama hii inaitupilia mbali tena kwa gharama pingamizi hilo la Dk. Slaa linalosema kuwa Rose hakuwa na haki ya kupinga ndoa yake kwa sababu hakuwa mke wake na wala hawajawahi kufunga ndoa kwa sababu sheria ya ndoa inasema mtu ambaye umeishawahi kuishi kama mke na mume kwa zaidi ya miaka miwili, inawahesabu kama ni wana ndoa.
“Hivyo mahakama hii inasema Rose ana haki ya kufungua kesi ya kuzuia ndoa ya wadaiwa, yaani Slaa na Josephine na natupilia mbali pingamizi la Slaa na kwamba kesi ya msingi itakuja kutajwa mahakamani hapa Novemba 6 mwaka huu,” alisema Jaji Kaduri.
Kesi hiyo ya madai ya ndoa ilifunguliwa mahakamani hapo na Rose dhidi ya Dk. Slaa na Josephine kwa mara ya kwanza mapema Julai mwaka huu, akiiomba mahakama isikubali shauri hilo lipelekwe kwenye Bodi ya Maridhiano ya Masuala ya Ndoa kwa ajili ya kupatanishwa.
Dai la pili, Rose anaiomba mahakama itangaze yeye na Dk. Slaa bado ni wanandoa, na dai la tatu anaiomba mahakama itamke kuwa ndoa baina yake na Dk. Slaa bado halali kisheria na kwamba ndoa nyingine itakayofungwa kinyume na sasa itakuwa ni batili. Katika dai lake la nne, mlalamikaji ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), anadai mdaiwa wa pili (Josephine) alimshawishi mumewe kuivuruga ndoa yake.
Pia nia ya wadaiwa hao wawili ya kutaka kufunga ndoa waliyopanga ifungwe Julai 21 mwaka huu katika eneo lolote lile, ndoa hiyo ihesabike kuwa ni batili.
Aidha, anaiomba mahakama iwaamuru wadaiwa wamlipe fidia ya shilingi milioni 50 kama gharama za matunzo ya watoto wawili ambao ni Emiliana Slaa na Linus Slaa aliyezaliwa mwaka 1987 ambao amekuwa akiwahudumia tangu mwaka 2009 baada ya mume wake kumkimbia.
Pia anaiomba mahakama imwamuru mdaiwa wa pili (Josephine) amlipe fidia ya sh mil. 500 kwa sababu alimsababishia usumbufu mkubwa na kumharibia ndoa yake, na kuongeza kwa kuiomba mahakama hiyo impatie nafuu nyingine ambazo itaona inafaa.

Jeshi, FFU wazima maandamano Dar • Zanzibar waharibu hosteli, wang’oa misalaba




JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) jana lililazimika kuingia mtaani katika jitihada za kuzima ghasia kubwa zilizoligeuza eneo zima la Kariakoo jijini Dar es Salaam kuwa uwanja wa mapambano.
Mapambano yalizuka baada ya kundi la wafuasi wa kiongozi wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, waliotaka kuandamana kuelekea Ikulu jijini Dar es Salaam kupinga kukamatwa kwa viongozi wao.
Askari wa JWTZ waliokuwa katika magari matano, wakiwa wamesheheni zana za kivita, waliwasili katika eneo la Kariakoo, na wengine kuelekea Ikulu kudhibiti maandamano ya wafuasi hao.
Rais Jakaya Kikwete aliyewasili Ikulu majira ya saa 7:48 mchana alilakiwa na ulinzi mkali wa askari wa JWTZ, huku mmoja wa wafuasi hao akiwa anashikiliwa na polisi.
Wafuasi hao pia walikuwa na chupa za maji, miswaki na sabuni ndani ya kanzu zao wakionekana kuwa tayari kwa lolote.
Vurugu hizo zilianza majira ya saa 7 mchana katika Mtaa wa Msimbazi jirani na Kituo cha Polisi, mara baada ya Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa katika Msikiti wa Idrisa, ambapo waumini hao waligawiwa vipeperushi vya kuwahimiza kuandamana kuelekea Ikulu.
Wafuasi hao walizidi kuongezeka baada ya kuungana na wenzao waliotoka katika Msikiti wa Kwamtoro na hivyo kufanya mapambano kuwa makali zaidi, huku baadhi ya watu wanaoaminika kuwa wezi na vibaka wakipora bidhaa mbalimbali za wafanyabiashara.
Ghasia hizo zilisababisha kusimama kwa shughuli zote za kijamii, na kulazimika kufungwa kwa barabara zote katika eneo hilo.
Wakati hali ikizidi kuwa tete, ndipo magari matano yaliyokuwa yamebeba askari wa JWTZ wakiwa na silaha za moto yaliwasili katika eneo hilo kwa mbwembwe.
Askari hao walionekana kuwa tayari kwa lolote, lakini hawakuweza kuanza mapambano yoyote wala kutumia silaha kukabiliana na wafuasi hao. Katika vurugu hizo zaidi ya watu 100 wamekamatwa.
Waandamanaji hao walikuwa wamebeba vipeperushi vilivyokuwa na maandishi ya kupinga kukamatwa kwa Waislamu na kuteswa, akina mama kudhalilishwa na kuwekwa ndani, misikiti kupigwa mabomu Mbagala, Polisi kuingia na viatu msikitini na kulaani hatua ya Rais Kikwete kuwapa pole Wakristo katika sakata la vurugu za Mbagala.
Mmoja wa wafuasi waliokamatwa katika eneo la Ikulu aliwaeleza askari waliomkamata kuwa alikuwa tayari kufa na kwenda peponi kwa madai kuwa alikuwa akishiriki vita ya jihadi kwa ajili ya Allah.
Zanzibar hakukaliki
Huko Zanzibar, hali ya usalama iliendelea kutoweka kufuatia kuongezeka kwa ghasia zinazoaminika kufanywa na wafuasi wa kundi la Uamsho.
Wafuasi wa kundi hilo juzi usiku walivamia makaburi ya Wakristo na kuyaharibu ikiwa ni pamoja na kubomoa misalaba, huku wakitishia kuchoma moto Kanisa la Anglikana.
Watu hao pia waliharibu hosteli inayomilikiwa na Kanisa la Anglikana Mkunazini, huku wakitishia kufanya uharibifu zaidi.
Kutokana na hali kuwa tete zaidi, baadhi ya wakazi wa Unguja ambao ni Wakristo wameanza kuukimbia mji huo, ambapo jana zaidi ya watu 60 waliwasili katika bandari ya Dar es Salaam.
Kuchafuka kwa hali hiyo kumeiweka Serikali ya Umoja wa Kitaifa katika wakati mgumu hasa kufuatia hatua ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka CCM kususia vikao vyake juzi wakipinga ghasia hizo na kuwataka wakuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Bara na Zanzibar kujiuzulu.
Mihadhara yapigwa marufuku
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiki, amepiga marufuku mihadhara yote ya dini mpaka hali ya usalama itakaporejea.
Alizungumza hayo jana katika mkutano uliowajumuisha Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC), Padri Anthony Makunde na kuzitaka mamlaka zote zinazoshughulika na utoaji vibali vya mihadhara hiyo kuacha kufanya hivyo.
Naye Padre Makunde alitoa rai kwa Watanzania kuendelea kuvumilia na kudumisha upendo na mshikamano uliopo miaka mingi baina yao na kusema kuwa njia pekee ya kufikia suluhu ni mazungumzo bila jazba na hasira.
Kwa upande wake Sheikh Alhad aliwataka Waislamu, maimamu na masheikh kuwa na subira na kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani na kutojidanganya kuwa na jihad kwani haiji kwa uvunjifu wa sheria na kwamba nidhamu ya dini hiyo na utaratibu wake unakataa vitendo hivyo.
Lwaitama aishukia serikali
Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Azavel Lwaitama, amesema udhaifu wa serikali ndio umefanya suala la vurugu za wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Kiislamu kulifikisha taifa hapa lilipo.
Udhaifu huo Lwaitama alisema ulianza tangu katika kipindi cha fujo za Mwembechai ambapo serikali haijaonesha jitihada zozote za kulitafutia suala hilo ufumbuzi.
Kutokana na hali hiyo, Lwaitama alitaka busara itumike zaidi katika kutatua fujo zinazoendelea sasa hivi badala ya kutumia nguvu kwani inaweza kuifikisha nchi pahali pasipotarajiwa.
Alisema kitendo cha kukamatwa kwa Sheikh Ponda sasa hivi na kusomewa mashitaka ya matukio yaliyotendeka tangu huko nyuma baada tu ya kuvamia kiwanja ni kama kutaka kuficha kitu nyuma ya pazia.
“Mimi naishangaa sana hii serikali kwani wakati matukio yale ya nyuma yalipotokea walikuwa wanashindwa nini kumkamata Sheikh huyo? Hebu katika hili busara zaidi itumike kwani na yeye ana wafuasi wake wengi hivyo watakapoamua kuingia barabarani hakuna atakayesalimika,” alisema.
Pia hakusita kuwapongeza viongozi wa madhehebu ya Kikristu kwa hatua yao walioichukua ya kuwa wavumilivu katika kipindi hiki na kukazana na maombi.
Kuhusu mtoto aliyekojolea msaafu, Lwaitama alisema hayo yote yametokana na matukio ya mfumo wa elimu uliopo sasa hivi hapa nchini wa kutoheshimu dini za wenzao.
Alisema umri wa mtoto huyo wa miaka 14 sio mdogo kihivyo kiasi cha kushindwa kutambua kile alichokuwa anakifanya ni kosa na badala yake alisema elimu wanayopewa watoto siku hizi haiwajengi katika kuweza kuishi na watu tofauti kwenye jamii.
Kova akanusha
Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi, Suleiman Kova amekanusha taarifa iliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Jeshi la Polisi limewataka Waislamu wote wa kikundi hicho kujisalimisha kwa jeshi hilo.
Kova alisema kuwa watu wanaotakiwa kujisalimisha ni sita na kuwataja kuwa ni Mukadam Saleh Kondo, Saleh Juma Bungo, Shaaban Mapeo, Jaafar Mneki, Rajab Katimba na Amani Moshi.
Hadi tunakwenda mitamboni, hali katika mitaa mingi ya Kariakoo ilikuwa haijatulia na kulikuwa na wasiwasi kwamba, watu hao walikuwa wakijikusanya kuendeleza mapambano na polisi.

Ikulu yamkana aliyemtesa Ulimboka






WAKATI sakata la kutekwa, kuteswa na kisha kutupwa katika msitu wa Mwabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar ss Salaam kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk Steven Ulimboka, likiwa limefikia miezi mitatu, Ikulu imeibuka na kumkana mtumishi wake Ramadhan Ighondu anayetajwa kuhusika katika unyama huo.
Mwanzoni mwa wiki Dk. Ulimboka alitoa tamko akisema kwamba Ighondu ndiye aliyehusika na sakata la kumteka na kumtesa vibaya katika jaribio la kutaka kumuua.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumamosi, Ikulu jana, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, alisema kuwa hamfahamu mtumishi huyo aliyetajwa na Ulimboka.
Alisisitiza kuwa Ikulu haipo kwa ajili ya kuteka na kutesa watu, hivyo wale wanaodai kuwa mtumishi wa ofisi hiyo anahusika na tukio hilo wanaongea tu.
“Wala simfahamu…Ikulu haipo kwa ajili ya kutesa watu na hao wanaomtaja mtumishi huyo kuwa yupo Ikulu hao wanazungumza tu,” alisema.
Wakati Balozi Sefue akitoa kauli hiyo, juzi Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alisisitiza kuwa Ikulu haihusiki na kwamba Rais Jakaya Kikwete alishalijibu suala hilo.
Katika tamko lake la kiapo lililotolewa kwa waandishi wa habari, Dk. Ulimboka, kupitia kwa wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheere, alisema anamfahamu mtesaji wake, na kwamba hata akikamatwa leo hii, atakwenda kufanya utambuzi.
Alisema anashangaa kwamba polisi wameshindwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, licha ya kwamba alishatajwa na gazeti la MwanaHALISI na katika mtandao wa YouTube.
Alisema: “Nathibitisha kwamba Ramadhan Ighondu alitambulishwa kwetu kwa jina la Abeid. Binafsi ninamfahamu sana bwana huyu kwa sababu alikuwa akitumwa mara kwa mara kuja kukutana na mimi na tumekutana mara kadhaa kabla ya tukio lile.
“Nathibitisha kwamba mfanyakazi huyu wa Ikulu, ndiye aliyenipigia simu na kuniita kwenye kikao ambacho muda mfupi baadaye nilitekwa. Katika mawasiliano hayo, Abeid alikuwa anatumia simu namba 0713 760473.”
Dk. Ulimboka aliongeza kuwa, anakumbuka kuwa Abeid alitambulishwa kwake na kigogo mmoja, akiwa na wawakilishi wengine wa madaktari, kuwa ndiye angehusika katika kuchukua madai na hoja za madaktari katika mgogoro kati yao na serikali.
Kauli ya jana ya Balozi Sefue ni ya tatu kutolewa na Ikulu kuhusu Dk. Ulimboka.
Mara ya kwanza, ilitolewa na Rais Jakaya Kikwete alipokutana na baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ambapo alisema, “Dk. Ulimboka ana nini mpaka Ikulu imteke? Tumteke ili iweje?”
Kikwete alikwenda mbali zaidi na kusema hata Dk. Ulimboka mwenyewe alipokwenda Ikulu akiwa na viongozi wenzake, alinyamaza kimya tu na kwamba waliokuwa wakizungumza ni wengine.
Hata hivyo, kwa kuwa Ikulu imesema haihusiki, na Dk. Ulimboka mwenyewe ametamka kwamba anamjua aliyemtesa, na kwamba anafanya kazi Ikulu, ni juu ya umma kuamua nani anasema ukweli.
Juni 26, mwaka huu, Dk. Ulimboka alitekwa, akapigwa, akang’olewa kucha kabla ya kuokotwa msitu wa Mabwepande na kupelekwa katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) kwa matibabu.
Hata hivyo, baadaye alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi na alirejea nchini Agosti 12, mwaka huu.

Monday, October 15, 2012

The Satanic Verses

From Wikipedia, the free encyclopedia
Jump to: navigation, search
The Satanic Verses
1988 Salman Rushdie The Satanic Verses.jpg
First edition cover
Author(s) Salman Rushdie
Country United Kingdom
Language English
Genre(s) Magic Realism, Novel
Publisher Viking Press
Publication date 1988
Media type Print (Hardback and paperback)
Pages 547 pp
ISBN 0-670-82537-9
OCLC Number 18558869
Dewey Decimal 823/.914
LC Classification PR6068.U757 S27 1988
Preceded by Shame
Followed by Haroun and the Sea of Stories
The Satanic Verses is Salman Rushdie's fourth novel, first published in 1988 and inspired in part by the life of Muhammad. As with his previous books, Rushdie used magical realism and relied on contemporary events and people to create his characters. The title refers to the so-called "satanic verses", a group of alleged Quranic verses that allow intercessory prayers to be made to three Pagan Meccan goddesses: Allāt, Uzza, and Manāt.[1] The part of the story that deals with the "satanic verses" was based on accounts from the historians al-Waqidi and al-Tabari.[1]
In the United Kingdom, the book received positive reviews. It was a 1988 Booker Prize Finalist (losing to Peter Carey's Oscar and Lucinda) and won the 1988 Whitbread Award for novel of the year.[2] The Satanic Verses sparked a major controversy when conservative Muslims accused it of blasphemy and mocking their faith. The outrage among some Muslims resulted in a fatwā calling for Rushdie's death issued by Ayatollah Ruhollah Khomeini, the Supreme Leader of Iran, on 14 February 1989. Although Rushdie himself has never been attacked as a result of the book's creation, Islamic extremists have attacked several connected individuals such as translator Hitoshi Igarashi (leading to, in Igarashi's case, death).

[edit] Plot

The Satanic Verses consists of a frame narrative, using elements of magical realism, interlaced with a series of sub-plots that are narrated as dream visions experienced by one of the protagonists. The frame narrative, like many other stories by Rushdie, involves Indian expatriates in contemporary England. The two protagonists, Gibreel Farishta and Saladin Chamcha, are both actors of Indian Muslim background. Farishta is a Bollywood superstar who specializes in playing Hindu deities. (The character is partly based on Indian film stars Amitabh Bachchan and Rama Rao.[3]) Chamcha is an emigrant who has broken with his Indian identity and works as a voiceover artist in England.
At the beginning of the novel, both are trapped in a hijacked plane flying from India to Britain. The plane explodes over the English Channel, but the two are magically saved. In a miraculous transformation, Farishta takes on the personality of the archangel Gibreel, and Chamcha that of a devil. Chamcha is arrested and passes through an ordeal of police abuse as a suspected illegal immigrant. Farishta's transformation can partly be read on a realistic level as the symptom of the protagonist's developing schizophrenia.
Both characters struggle to piece their lives back together. Farishta seeks and finds his lost love, the English mountaineer Allie Cone, but their relationship is overshadowed by his mental illness. Chamcha, having miraculously regained his human shape, wants to take revenge on Farishta for having forsaken him after their common fall from the hijacked plane. He does so by fostering Farishta's pathological jealousy and thus destroying his relationship with Allie. In another moment of crisis, Farishta realizes what Chamcha has done, but forgives him and even saves his life.
Both return to India. Farishta kills Allie in another outbreak of jealousy and then commits suicide. Chamcha, who has found not only forgiveness from Farishta but also reconciliation with his estranged father and his own Indian identity, decides to remain in India.

[edit] Dream sequences

Embedded in this story is a series of half-magic dream vision narratives, ascribed to the mind of Gibreel Farishta. They are linked together by many thematic details as well as by the common motifs of divine revelation, religious faith and fanaticism, and doubt.
One of these sequences contains most of the elements that have been criticized as offensive to Muslims. It is a transformed re-narration of the life of Muhammad (called "Mahound" or "the Messenger" in the novel) in Mecca ("Jahilia"). At its centre is the episode of the so-called satanic verses, in which the prophet first proclaims a revelation in favour of the old polytheistic deities, but later renounces this as an error induced by Shaitan. There are also two opponents of the "Messenger": a demonic heathen priestess, Hind, and an irreverent skeptic and satirical poet, Baal. When the prophet returns to the city in triumph, Baal goes into hiding in an underground brothel, where the prostitutes assume the identities of the prophet's wives. Also, one of the prophet's companions claims that he, doubting the "Messenger"'s authenticity, has subtly altered portions of the Quran as they were dictated to him.
The second sequence tells the story of Ayesha, an Indian peasant girl who claims to be receiving revelations from the Archangel Gibreel. She entices all her village community to embark on a foot pilgrimage to Mecca, claiming that they will be able to walk across the Arabian Sea. The pilgrimage ends in a catastrophic climax as the believers all walk into the water and disappear, amid disturbingly conflicting testimonies from observers about whether they just drowned or were in fact miraculously able to cross the sea.
A third dream sequence presents the figure of a fanatic expatriate religious leader, the "Imam," in a late-20th-century setting. This figure is a transparent allusion to the life of Ayatollah Khomeini in his Parisian exile, but it is also linked through various recurrent narrative motifs to the figure of the "Messenger".

[edit] Literary criticism and analysis

Overall, the book received favourable reviews from literary critics. In a 2003 volume of criticism of Rushdie's career, influential critic Harold Bloom named The Satanic Verses "Rushdie's largest aesthetic achievement".[4]
Timothy Brennan called the work "the most ambitious novel yet published to deal with the immigrant experience in Britain" that captures the immigrants' dream-like disorientation and their process of "union-by-hybridization". The book is seen as "fundamentally a study in alienation."[2]
Muhammd Mashuq ibn Ally wrote that "The Satanic Verses is about identity, alienation, rootlessness, brutality, compromise, and conformity. These concepts confront all migrants, disillusioned with both cultures: the one they are in and the one they join. Yet knowing they cannot live a life of anonymity, they mediate between them both. The Satanic Verses is a reflection of the author’s dilemmas." The work is an "albeit surreal, record of its own author's continuing identity crisis."[2] Ally said that the book reveals the author ultimately as "the victim of nineteenth-century British colonialism."[2] Rushdie himself spoke confirming this interpretation of his book, saying that it was not about Islam, "but about migration, metamorphosis, divided selves, love, death, London and Bombay."[2] He has also said "It’s a novel which happened to contain a castigation of Western materialism. The tone is comic."[2]
After the Satanic Verses controversy developed, some scholars familiar with the book and the whole of Rushdie's work, like M. D. Fletcher, saw the reaction as ironic. Fletcher wrote "It is perhaps a relevant irony that some of the major expressions of hostility toward Rushdie came from those about whom and (in some sense) for whom he wrote."[5] He said the manifestations of the controversy in Britain "embodied an anger arising in part from the frustrations of the migrant experience and generally reflected failures of multicultural integration, both significant Rushdie themes. Clearly, Rushdie's interests centrally include explorations of how migration heightens one's awareness that perceptions of reality are relative and fragile, and of the nature of religious faith and revelation, not to mention the political manipulation of religion. Rushdie's own assumptions about the importance of literature parallel in the literal value accorded the written word in Islamic tradition to some degree. But Rushdie seems to have assumed that diverse communities and cultures share some degree of common moral ground on the basis of which dialogue can be pieced together, and it is perhaps for this reason that he underestimated the implacable nature of the hostility evoked by The Satanic Verses, even though a major theme of that novel is the dangerous nature of closed, absolutist belief systems."[5]
Rushdie's influences have long been a point of interest to scholars examining his work. According to W. J. Weatherby, influences on The Satanic Verses were listed as Joyce, Italo Calvino, Kafka, Frank Herbert, Pynchon, Mervyn Peake, Gabriel Garcia Marquez, Jean-Luc Godard, J. G. Ballard, and William Burroughs.[6] Chandrabhanu Pattanayak notes the influence of William Blake's The Marriage of Heaven and Hell and Mikhail Bulgakov's The Master and Margarita (influences Rushdie admitted to).[5] M. Keith Booker likens the book to James Joyce's Finnegans Wake.[5] Al-'Azm notes the influence of François Rabelais' works.[5] Others have noted an influence of Indian classics such as the Mahabharata and the Arabic Arabian Nights.[5] Angela Carter writes that the novel contains "inventions such as the city of Jahilia, 'built entirely of sand,' that gives a nod to Calvino and a wink to Frank Herbert".[7]
Srinivas Aravamudan’s analysis of The Satanic Verses was perceived by other scholars as hailing the book as a proof "demonstrating the compatibility of postmodernism and post-colonialism in the one novel."[5] Aravamudan himself stressed the satiric nature of the work and held that while it and Midnight's Children may appear to be more "comic epic", "clearly those works are highly satirical" in a similar vein of postmodern satire pioneered by Joseph Heller in Catch-22.[5]
The Satanic Verses continued to exhibit Rushdie's penchant for organizing his work in terms of parallel stories. Within the book "there are major parallel stories, alternating dream and reality sequences, tied together by the recurring names of the characters in each; this provides intertexts within each novel which comment on the other stories."[5] The Satanic Verses also exhibits Rushdie's common practice of using allusions in order to invoke connotative links. Within the book he referenced everything from mythology to "one-liners invoking recent popular culture" sometimes using several per page.[5] Chapter VII was especially noted by for such usage.[5]

[edit] Controversy

The novel caused great controversy in the Muslim community for what some Muslims believed were blasphemous references. Rushdie was accused of mis-using freedom of speech.[8] As the controversy spread, the import of the book was banned[9] in India and it was burned in demonstrations in the United Kingdom. In mid-February 1989, following a violent riot against the book in Pakistan, the Ayatollah Ruhollah Khomeini, Supreme Leader of Iran and a Shi'a Muslim scholar, issued a fatwa calling on all good Muslims to kill Rushdie and his publishers, or to point him out to those who can kill him if they cannot themselves.[10] Although the British Conservative government under Margaret Thatcher gave Rushdie round-the-clock police protection, many politicians on both sides were hostile to the author. British Labour MP Keith Vaz led a march through Leicester shortly after he was elected in 1989 calling for the book to be banned, while Conservative MP Norman Tebbit, the party's former chairman, called Rushdie an "outstanding villain" whose "public life has been a record of despicable acts of betrayal of his upbringing, religion, adopted home and nationality".[11] Meanwhile the Commission for Racial Equality and a liberal think tank, the Policy Studies Institute held seminars on the Rushdie affair. They did not invite the author Fay Weldon who spoke out against burning books, but did invite Shabbir Akhtar, a Cambridge philosophy graduate who called for "a negotiated compromise" which "would protect Muslim sensibilities against gratuitous provocation". The journalist and author Andy McSmith wrote at the time "We are witnessing, I fear, the birth of a new and dangerously illiberal "liberal" orthodoxy designed to accommodate Dr Akhtar and his fundamentalist friends."[12]
Following the fatwa, Rushdie was put under police protection by the British government. Despite a conciliatory statement by Iran in 1998, and Rushdie's declaration that he would stop living in hiding, the Iranian state news agency reported in 2006 that the fatwa would remain in place permanently since fatwas can only be rescinded by the person who first issued them, and Khomeini had since died.[13]
Rushdie has never been physically harmed for the book, but others associated with it have suffered violent attacks. Hitoshi Igarashi, its Japanese translator, was stabbed to death on 11 July 1991. Ettore Capriolo, the Italian translator, was seriously injured in a stabbing the same month.[14] William Nygaard, the publisher in Norway, was shot three times in an attempted assassination in Oslo in October 1993, but survived. Aziz Nesin, the Turkish translator, was the intended target in the events that led to the Sivas massacre on 2 July 1993 in Sivas, Turkey, which resulted in the deaths of 37 people.[15] Individual purchasers of the book have not been harmed. The only nation with a predominantly Muslim population where the novel remains legal is Turkey.[citation needed]
In September 2012, Rushdie expressed doubt that The Satanic Verses would be published today because of a climate of "fear and nervousness".[16]

Mwakyembe apangua wakurugenzi uchukuzi




WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, amewapangua wakurugenzi wa idara mbalimbali ndani ya wizara yake lengo likiwa kuboresha ufanisi ndani ya wizara hiyo.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Dk Mwakyembe alisema , kubadilisha watendaji ni mchakato ambao upo serikalini na hata hivyo waliokuwa katika nafasi hizo walikuwa wakikaimu.

"Tumeweka wahusika kamili kwa nafasi zao, tunataka kuleta ufanisi wa utendaji ndani ya Wizara," alisema Mwakyembe.

Katika panguapangua hiyo, Wakurugenzi wakuu na wasaidizi 14 ndiyo waliokumbwa na hatua hiyo.

Taarifa ya Wizara iliyotiwa saini na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Omar Chambo, imewataja walioteuliwa kuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa miundombinu na usafiri, Mhandisi Edwino Mujwahuzi.

Wengine walioteuliwa na nafasi zao kwenye mabano ni Peter Lupatu (Idara ya huduma na usafirishaji) na Gabriel Migire atakayeongozaiIdara ya Ssra na mipango.

Pia yumo Festo Mwanyika (Mkurugenzi msaidizi, huduma za usafiri wa reli) na Aron Kisaka atakayekuwa Mkurugenzi msaidizi, huduma ya usafiri wa barabara.

Deogratius Mukasa atakuwa Mkurugenzi msaidizi wa huduma za safiri wa majini wakati Hilal Ali Mohamed ameteuliwa wadhifa wa Mkurugenzi msaidizi miundombinu ya reli.

Wengine ni Injinia Rugera Majula (Mkurugenzi msaidizi, miundombinu ya Viwanja vya Ndege) na Aminel Hassan Omar  aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi msaidizi wa miundombinu ya bandari.

Chambo aliwataja wengine kuwa ni Erasto Wapalila (Mkurugenzi msaidizi wa ulinzi na usalama wa usafirishaji na Aunyisa Meena atakayekuwa Mkurugenzi msaidizi wa usimamizi, ufuatiliaji na tathimini.

Wengine walioteuliwa kwa mujibu wa taarifa hiyo ni Sifael Sekei (Mkurugenzi msaidizi, mazingira na huduma za jamii) na Edward Mkiaru anayekuwa Mkurugenzi msaidizi wa sera.

Aidha katika uteuzi huo, Abdulrahaman Said Mbamba ameteuliwa kuwa Mkuu wa kitengo cha teknolojia ya habari na mawasiliano.

“Tumeteua wakurugenzi na wakurugenzi wasaidizi wapya kwa lengo la kuimarisha utendaji katika wizara hiyo, wananchi watarajie ufanisi bora wa kazi,î ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Mabadiliko hayo yamekuja ikiwa ni miezi minne tangu Dk  Mwakyembe amsimamishe kazi bosi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), Paul Chizi kutokana na tuhuma za ufisadi.

Aidha mabadiliko hayo yamekuja ikiwa ni miezi miwili na nusu tangu Dk Mwanyembe amsimamishe kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraem Mgawe kutokana na matumizi mabaya ya ofisi yake.

Kifo cha Daud Mwangosi bado ni kitendawili



KAMATI iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi kuchunguza kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi juzi ilikabidhi ripoti yake kwa waziri huyo, lakini kwa mshangao wa wengi ripoti hiyo ilibakia kuwa siri ya Serikali kwa maelezo kuwa, kesi ya mauaji hayo tayari iko mahakamani na kwamba  kuiweka hadharani kungegusa mambo ambayo yangeingilia  mwenendo wa kesi hiyo.
Badala yake vyombo vya habari vilipewa kile Kamati hiyo ilichokiita Muhtasari wa Uchunguzi wa Kifo cha Mwangosi wenye kurasa 10 za maelezo ya jumla tu na yenye kujirudiarudia, tena mara nyingine kwa mafumbo. Kwa mfano, katika muhtasari wake, Kamati hiyo iliyokuwa chini ya Jaji mstaafu Steven Ihema ilipendekeza nafasi za wakuu wa wilaya na mikoa ‘ziangaliwe upya’ kwa maelezo kwamba zinatumika kisiasa. Hapa maana ya nafasi hizo kuangaliwa upya ni kama fumbo analofumbiwa mjinga.
Hata hivyo, pamoja na muhutasari wa ripoti hiyo kuelekeza lawama kwa baadhi ya watu wasiohusika, sehemu ya muhtasari wa ripoti hiyo imetenda haki. Kwa mfano, pamoja na mambo mengine, sehemu hiyo inasema nguvu iliyotumiwa na polisi kuwatawanya wafuasi wa Chadema siku ya tukio ilikuwa kubwa kupita kiasi na kuwa, licha ya kwamba utumiaji wa mabomu haukufanywa kwa weledi, pia matumizi ya silaha hizo  hayakuwa ya lazima.
Hali hiyo iliamsha ghadhabu ya wananchi wengi ambao kupitia katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii waliituhumu Serikali kwamba ilikuwa inaficha ukweli kuhusu kifo hicho kwa kuzingatia kwamba kesi za aina hiyo hutumia miaka nyingi kutolewa hukumu. Kwa maana hiyo, wananchi walihisi kwamba huo ndiyo ulikuwa mwisho wa matumaini yao ya kupata undani wa kifo cha mwanahabari  huyo aliyeuawa akiwa mikononi mwa polisi.
Lakini ghadhabu ya wananchi ilichochewa na ripoti za kamati nyingine tofauti zilizoundwa katika nyakati tofauti kuchunguza mazingira ya kifo cha mwandishi huyo kutokana na vurugu zilizotokea Septemba 2 mwaka huu katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi mara baada ya polisi kuwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakifungua tawi la chama hicho katika kijiji hicho.
Baraza la Habari Tanzania (MCT), nalo juzi lilianika ripoti yake kuhusu kifo hicho ambayo ilisema mauaji hayo yalifanywa na polisi kwa makusudi kutokana na uhasama ambao umekuwapo kwa muda mrefu baina ya waandishi na polisi mkoani Iringa. Pia ripoti hiyo ilisema mwandishi huyo aliuawa mikononi mwa polisi chini ya usimamizi wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda na kwamba hiyo inathibitishwa na maelezo pamoja na ushahidi uliokusanywa kwa kutumia picha  za video na ushahidi mwingine muhimu wa taarifa za vyombo vya habari.
Wakati hayo yakitokea, Tume ya Haki za Binadamu jana ilizindua ripoti yake kuhusu mauaji ya mwandishi huyo na kumlaumu Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Michael Kamuhanda na kusema kupitia kwa mwenyekiti wake, Jaji Kiongozi mstaafu, Amiri Manento kwamba alikosea kisheria kutengua amri ya  Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi ambaye awali alikuwa ametoa kibali kwa Chadema kufanya shughuli ya kufungua matawi ya chama hicho pasipo kufanya maandamano.
Taasisi nyingi zimetoa kauli za kukosoa Serikali na Kamati ya Jaji Ihema kwa kuficha ripoti hiyo. Kwa mfano, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema kukataa kutoa ripoti hiyo hadharani na badala yake kutoa muhtasari wake ni makosa makubwa ambayo hayasahameki.
Pamoja na kukiri kwamba Kamati hiyo iliyoteuliwa na Waziri Nchimbi imefanya kazi nzuri katika baadhi ya maeneo, tunalazimika kusema kwamba ilipaswa kuishauri Serikali kuitoa ripoti hiyo hadharani badala ya kuishauri kuificha kabatini kwa kisingizio cha kesi iliyopo mahakamani. Tunadhani kwamba hatua hiyo imewanyima wananchi fursa ya kupata habari na hakika huo siyo utawala bora.

Wataka madaraka ya rais yapunguzwe





WAKAZI wa Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, wametaka katiba mpya ijayo, madaraka ya rais wa nchi ya kuteua watendaji wakuu yaangaliwe upya na ikiwezekana yapunguzwe.
Wakitoa maoni yao juzi katika mdahalo wa katiba mpya ulioendeshwa na Mtandao wa asasi za kiraia Mkoa wa Lindi (Lango), wakazi hao walilishukuru shirika hilo kuwapa nafasi hiyo ya kutoa maoni kutokana na kuikosa wakati tume ya kukusanya maoni ilipopita mkoani humo hivi karibuni.
Mmoja wa wakazi hao, Mawazo Hashimu mkazi wa Nachingea, alisema kuwa katika katiba ijayo, iko haja ya rais kupunguziwa madaraka ya kuwateua watendaji na kuwepo na ukomo wa madaraka.
“Rais asiwateue wabunge kuwa mawaziri, kwani hao ni watetezi wa wananchi na wawakilishi wao bungeni… sasa rais atakapowateua kuwa mawaziri hawatapata muda wa kuwatetea wale waliowachagua,” alisema.
Aidha, wananchi hao walipendekeza kuwepo na ukomo wa madaraka ya viongozi kwani wamekuwa wakiongoza nchi kwa miaka 30 hadi 40.
Wananchi hao waliongeza kuwa katiba hiyo iwabane wabunge kuishi majimboni kwao kama ilivyo kwa madiwani badala ya sasa ambapo wengi wao wamekimbia majimboni na kuhamia jijini Dar es Salaam.

Kada CCM amkomalia Sumaye


KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM), David Msuya, amemtaka Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, kuwataja waliotoa rushwa katika uchaguzi wa viongozi wa CCM mwaka huu.
Msuya ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Sumaye kueleza sababu zilizochangia ashindwe uchaguzi wa nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, wilaya ya Hanang, kuwa unatokana na vitendo vya rushwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msuya ambaye pia ni mkurugenzi wa vikundi vya maendeleo ya wanawake (Inuka), alisema badala ya kulalamika, Sumaye anatakiwa awataje wala rushwa na watoa rushwa walioko ndani ya chama hicho, ili wachukue hatua kwa mujibu wa sheria.
“Sisi Watanzania hatupendi rushwa maana ni adui wa haki, hivyo si busara kuongea tu badala ya kuchukua hatua kwa kuwa yeye ni kiongozi mkubwa mwenye sauti serikalini ambaye kama analalamika na sisi tufanyeje? Kwa hiyo anatakiwa kupeleka suala hilo kwenye vikao vya chama,” alisema.
Aidha, Msuya aliitaka serikali ikae na viongozi wote wa dini katika kukemea vitendo vya vurugu vinavyoweza kujitokeza na kuharibu amani ya nchi kutokana na vurugu za kidini zilizoibuka hivi karibuni ambapo makanisa na vitu mbalimbali ama vimechomwa moto au vimeibiwa.

JK: Vurugu za kidini Mbagala zinaudhi






RAIS Jakaya Kikwete, amesema kuwa licha ya tukio la kijana wa Kikristo kukojolea kitabu kitakatifu cha Kuran kuudhi, lakini vurugu za kulipiza kisasi kwa kuchoma makanisa zinapaswa kuepukwa kwa vile si suluhu ya tatizo.
Akihutubia katika kilele cha kuzima Mwenge wa Uhuru, sherehe zilizokwenda sambamba na kumbukumbu za maadhimisho ya miaka 13 ya kifo cha Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, mjini Shinyanga, Rais Kikwete alisema amechukizwa na hatua za watu kujichukulia sheria mkononi.
Kauli ya rais inakuja ikiwa ni siku tatu tangu vurugu kubwa kutokea eneo la Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam na kusababisha makanisa saba na magari kadhaa kuharibiwa, baada ya mtoto Emmanuel Josephat (14) kudaiwa kukojolea kitabu hicho kitakatifu kinachotumiwa na Waislamu.
Rais Kikwete aliwaeleza wananchi kuwa ametembelea eneo hilo na kusisitiza kuwa kitendo hicho cha viongozi wa dini kuwahamasisha wafuasi wao kujichukulia sheria mkononi hakikuwa sahihi, kwa sababu kijana huyo alifanya tendo hilo bila kushurutishwa na kundi wala mtu yeyote.
Aliongeza kuwa iko haja ya wafuasi hao kujizuia na kutuliza hasira zao kwa kutafakari kwanza kwani hata kijana mwenyewe tayari alikuwa mikononi mwa Jeshi la Polisi.
“Kitendo cha kundi hilo la waumini wa Kiislamu kuingilia kazi za vyombo vya dola hakikuwa sahihi, kwa sababu kimesababisha mambo ya kusikitisha na yasiyokuwa na maelezo ya kujitosheleza ndani ya jamii.
“Niliwasihi kuwa pamoja na hasira walizokuwa nazo wawe na subira na kuvumiliana wakati viongozi wa dini zote mbili wanapojiandaa kukutana na kufikia muafaka,” aliongeza.
Rais Kikwete aliwataka wananchi wajiepushe na vitendo vya kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani katika nchi, hivyo akawashauri wasichukue uamuzi wa hasira wakati wa tatizo kwa sababu kwa vyovyote vile ni lazima watadondokea kwenye makosa.
Alisema vijana 122 wanaodaiwa kutoka kundi la harakati za Kiislamu wakiwemo 36 vinara wakuu wa vurugu hizo, wanashikiliwa na polisi.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete aliwahamasisha Watanzania kuendelea kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao kwenye tume inayoratibu maoni bila kushawishiwa kwa ulaghai wa aina yoyote, kwamba hiyo ni haki na utashi wa kila mtu.
Akemea rushwa
Rais Kikwete katika hilo, aliwataka wananchi wote kuchukua jukumu la kupambana na vitendo vya rushwa pasipo kuwaachia kazi hiyo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Alisema vita hiyo ni ya kila mtu huku akiwapiga vijembe wale wanaolalamika uwepo wa vitendo hivyo pasipo kuchukuwa jukumu la kuwataja hadharani wahusika ili wachukuliwe hatua.
“Kama tunaendelea kulalamikia rushwa bila kuwataja wala rushwa haiwezi kutusaidia kuitokomeza. Rushwa ni hatari hasa inapoingia hata kwenye vyombo vya kusimamia sheria na kutoa haki,” alisema.
CCM watoa kauli
Wakati huo huo, Chama Cha Mapinduzi, kupitia kwa Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kimelaani vurugu za kidini zilizotokea Mbagala Kizuiani.
Alisema kuwa CCM kinalaani tukio la kukojelewa kwa kitabu kitakatifu cha Kuran na vile vile vitendo vya kuvamiwa na kuchomwa moto makanisa na uporaji wa mali, akisisitiza kuwa havifanani na mila na desturi za Watanzania.
“Kitendo cha kukojolea kitabu kitakatifu cha Waislamu hakikubaliki, na kitendo cha kuvamia na kuchoma moto nyumba za ibada za Wakristo na kufanya vurugu pia hakikubaliki,” alisema

Makongoro Nyerere agaragazwa CCM • JK aombwa kutengua ushindi wa waliotoa rushwa



MTOTO wa Baba wa Taifa, Makongoro Nyerere, ameangushwa katika kinyang’anyiro cha kutetea nafasi yake ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, ambayo sasa imechukuliwa na Christopher Sanya.
Makongoro ambaye amekuwa mwenyekiti wa mkoa huo kwa miaka mitano, alishindwa katika uchaguzi huo uliofanyika juzi chini ya usimamizi wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa kutoka Mkoa wa Kagera, Nasir Karamagi.
Akitangaza matokeo ya awali, Karamagi alisema kuwa kati ya kura 1,012 zilizopigwa, Sanya alipata 469 na Makongoro alijikusanyia 402 huku Enock Chambili akiambulia 144.
Lakini kwa mujibu wa Katiba ya CCM mshindi hakuwa amevuka nusu ya kura, na hivyo ilibidi Sanya na Makongoro, kuingia katika duru ya pili ambapo mwenyekiti huyo anayemaliza muda wake alipitwa kwa kura 59.
Akizungumza baada ya matokeo kutangazwa, Makongoro alimuasa Sanya kufanya kazi kwa mujibu wa katiba ya chama na kuvunja makundi yaliyoshamiri ndani ya CCM huku akiahidi kutoa ushirikiano wake.
“Naomba uwe muadilifu, mkoa huu wa Mara ni mgumu sana kuufanyia kazi, kwani kazi ya uenyekiti si lelemama, hii ndiyo nafasi kubwa ambayo itatusaidia katika uchaguzi wa 2014/2015,” alisema.
Makongoro aliwataka pia wajumbe kuachana na mambo ya kambi, akisema uchaguzi umekwisha kilichopo ni kushikamana na kuwapa ushirikiano viongozi wapya wakiongoze chama vizuri.
Katika nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM mkoa - kila wilaya nafasi mbili, waliopenya ni Josephat Seronga na Ester Nyarobi (Serengeti), Zuhura Makongoro na Jackson Waryoba (Bunda), Josehat Kisusi na Felister Nyambaya (Rorya).
Wengine ni Grace Bunyinyiga na Thabita Idd (Butiama), Abdalah Jumapili na Kananda Kananda (Musoma Mjini) na Mariam Mkono na Samson Gesase (Tarime).
Kamani ang’ara Simiyu
Mbunge wa Busega, Dk. Titus Kamani, amepata ushindi wa kishindo katika kinyanganyiro cha uenyekiti Mkoa mpya wa Simiyu baada ya kujizolea kura 415.
Waliobwagwa ni aliyekuwa Mbunge wa Afrika Mashariki, George Nangale na Mwenyekiti mstaafu wa CCM Wilaya ya Meatu, Enock Yacob.
Msimamizi wa uchaguzi huo, Jackson Msome, alisema kuwa kati ya kura 714 zilizopigwa, mbali na Dk. Kamani, Nangale alipata 234 huku Enock akiambulia 91.
Wakasuvi arejea Tabora
Mwenyekiti CCM Mkoa wa Tabora aliyemaliza muda wake, Hassan Wakasuvi, amefanikiwa kutetea kiti hicho kwa ushindi wa kishindo.
Wakasuvi aliwamwaga wenzake watatu ambao ni Zuberi Mwamba, Juma Nkumba na Haji Bagio ambao walijitoa muda mfupi kabla ya uchaguzi kuanza.
Akitangaza matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi huo, Mwigulu Mchemba, alisema kati ya kura 996 zilizopigwa, Wakasuvi alipata 921, akifuatiwa na Zuberi Mwamba kura 75 na 16 ziliharibika.
Katika nasaha zake, Wakasuvi aliwataka wajumbe wavunje makundi na wamsaidie kukijenga chama, huku akiahidi kushirikiana na kila mmoja bila kujali makovu ya uchaguzi.
Alionya kuwa wapo watu ambao wanadhani kwamba bila wao CCM Tabora haipo, akisema atawachukulia hatua maana ndani ya chama wamekuwa wakiketi vikao vya kukibomoa.
Msukuma apeta Geita
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Joseph Msukuma, aliyeng’olewa madarakani na Baraza la Madiwani kwa tuhuma za ufisadi, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa CCM Mkoa mpya wa Geita.
Katika uchaguzi huo, Msukuma alipata kura 565 kati ya 698 zilizopigwa na wajumbe wa wilaya tano za Nyang'hwale, Geita, Chato, Mbogwe na Bukombe zinazounda mkoa huo.
Msukuma aliwabwaga Jeremiah Ikangala, aliyepata kura 130 na Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo aliyemaliza muda wake, John Luhemeja aliyeambulia kura tano.
Mlao arudi Pwani
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, aliyemaliza muda wake, Mwinshehe Mlao, amefanikiwa kutetea kiti chake baada ya kuibuka na ushindi wa kura 528 dhidi ya Kapteni Mpembenue Seif Ally aliyepata kura 196 na Mziwanda Yahaya aliyeambulia 13.
Washindi wa ujumbe wa NEC kutoka wilayani ni Halfan Mavala, Asia Madima (Kibaha Vijijini), Fatma Ngozi, Mwajuma Denge (Bagamoyo), Hafsa Kilingo, Imani Madega (Kibaha Mjini) na Bakari Mbonde, Hawa Mtopa (Rufiji).
Kingunge anena
Kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru, amesema kuwa vitendo vya rushwa ndani ya chama hicho, vimeshamiri kutokana na ubinafsi wa baadhi ya wanachama kuweka mbele maslahi binafsi.
Mzee Kingunge, alitoa kauli hiyo juzi mkoani Pwani, wakati akifungua mkutano wa uchaguzi wa mkoa wa chama hicho, akisema kuwa ubinafsi huo umefanya vyama kuwa mali ya mtu na ushindani unakuwa si wa kindugu bali uhasama.
Alisema wakati wa Afro- Shiraz na TANU, nchi iliwekwa mbele tofauti na sasa ambapo ubinafsi ndio unawekwa mbele na nchi inabaki peke yake.
“Kwa kuwa suala ni ubinafsi ndiyo maana sasa watu wanafikia hatua ya kununua vyeo kutoka kwa wapiga kura, jambo linalomdhalilisha mtoaji na mpokeaji wa rushwa,”alisema.
JK ashauriwa
Mmoja wa wagombea wa Ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa ya CCM kupitia Wilaya ya Bunda, Cyprian Musiba, amemshauri Mwenyekiti wa chama, Rais Jakaya Kikwete, kuwafutia matokeo baadhi ya wagombea waliopita kwa rushwa.
Musiba ambaye ni mwanahabari kitaaluma na Mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya I&RH, alitaja nafasi ambazo Rais Kikwete anapaswa kutengua matokeo yake kuwa ni ya Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara na Morogoro.
Pia Musiba alitaja washindi wa nafasi ya ujumbe wa NEC katika wilaya za Monduli, Bunda na Musoma Mjini pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mara.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Musiba alifafanua kuwa wenye fedha wameifanya CCM kuwa sehemu ya kufichia madhambi yao, hivyo hawaoni hatari kutumia gharama yoyote kupata uongozi.
“Penye rushwa hakuna haki, hakuna kuwatumikia wananchi, mimi ni miongoni mwa wagombea nilioshuhudia hali hii, watu kutoa fedha kwa ajili ya kununua uongozi ni jambo la kawaida kwa CCM. Mkoani mara zimetumika zaidi ya milioni 300 kwa ajili ya kumwangusha Makongoro,” alisema Musiba.
Kada huyo ambaye wiki iliyopita aliwasilisha malalamiko yake ndani ya chama kupinga uchaguzi aliyoshiriki wilayani Bunda, alishauri kuwa rufaa hizo hazipaswi kusikilizwa na kamati za siasa na maadili za wilaya kwa vile wajumbe wake ndio watuhumiwa.
Alisisitiza kuwa katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara, fedha zilikuwa zikigawiwa wazi wazi kwa wajumbe na baadhi ya vigogo na wafanyabiashara wakubwa kuhakikisha watu wao wanashinda.
“Viongozi wanaotumia fedha ndani ya CCM hawawezi kuwa watetezi wa wanyonge. Na kwa rushwa hii hata uchaguzi wa Bunda kanuni zilikiukwa kwa kuruhusu mfanyakazi wa serikali kugombea,” alisema.
Musiba alisema kuwa anaungana na kauli ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ya kutaka wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi ndani ya CCM wawajibishwe kwa kutoswa.
Alisema ni fursa nzuri kwa NEC mpya aliyosema ina sura nyingi ngeni kutomuonea mtu aibu kwa lengo la kukinusuru chama kutokana na kutekwa na mafisadi hali aliyosema inazidi kukiangamiza.

Mnyika: Spika aunde Kamati ya Gesi

WAZIRI Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, amemtaka Spika wa Bunge, Anna Makinda, kutumia madaraka na mamlaka yake kutangaza kwa umma kamati nyingine ya kudumu ya Bunge itakayoshughulikia masuala ya gesi asili kabla na wakati wa mkutano wa Bunge ujao mwishoni mwa mwezi huu.
Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA, alisema hatua hiyo ni kutokana na hali tete na tata kuhusu sekta ndogo ya gesi asilia nchini na kwa kuzingatia umuhimu na unyeti wa sekta hiyo katika uchumi wa nchi na maisha ya wananchi.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mnyika alisema pamoja na mambo mengine, Spika Makinda aelekeze kamati hiyo kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge ya mwaka 2011 kuhusu sekta ndogo ya gesi asili ikiwemo juu ya hatua iliyofikiwa katika kushughulikia tuhuma za ufisadi.
Madai mengine ni ya mapunjo ya fedha za mauzo ya gesi asili na hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya sera, mpango mkakati na sheria ya gesi asili.
“Hatua hii ni muhimu kufuatia ukimya wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo kuhusu kauli yangu ya Oktoba 4, 2012 ya kutaka taarifa ya ufafanuzi kuhusu utafutaji wa mafuta na gesi asili nchini iliyotolewa na wizara hiyo Septemba 21 mwaka huu ifutwe,” alisema.
Alisema kuwa taarifa hiyo ya wizara ilieleza kuwa maandalizi ya sera ya gesi asili yapo katika hatua za mwisho wakati ambapo kamati mbalimbali za kudumu za Bunge hazijahusishwa katika mchakato huo muhimu pamoja na kuwa mamlaka ya kutunga sera kwa mfumo wa sasa ni ya Baraza la Mawaziri.
“Kwa unyeti na upekee wake sera ya gesi, Spika wa Bunge anapaswa kuwezesha Kamati za Kudumu za Bunge zihusishwe ili pawepo mashauriano na maridhiano kwa mapana na marefu,” alisema.
Mnyika alisema izingatiwe kwamba katika mkutano wa nane wa Bunge, Spika alitangaza kuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imevunjwa na kwamba majukumu iliyokuwa ikishughulikiwa yatashughulikiwa na kamati nyingine kwa mujibu wa madaraka na mamlaka ya spika.

Silaa: Wananchi timizeni wajibu

MEYA wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, amesema wananchi wanatakiwa kutimiza wajibu wao, ili nchi ipate maendeleo kwa haraka.
Amesema kama kila mmoja atatimiza wajibu wake na kuondokana na tabia ya kuitegemea serikali ifanye kila kitu, nchi itapata maendeleo haraka tofauti na inavyotarajiwa.
Silaa alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga maonesho ya kifedha na uwekezaji yaliyokuwa yakizishirikisha taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za kifedha.
“Maonesho haya yamefanyika kwa mara ya kwanza nchini, lakini naamini washiriki wote wamefika hapa kama sehemu ya kila mmoja kutimiza wajibu wake.
“Kila mmoja akitimiza wajibu wake naamini nchi itasonga mbele, kwa hiyo, tuondokane na tabia ya kuitegemea serikali katika kila jambo kwa sababu serikali ina mambo mengi,” alisema Silaa.
Naye Meneja Matukio wa Kampuni ya Neubrand iliyoandaa maonesho hayo, Geofrey Kivamba, alisema waliamua kuandaa maonesho hayo, ili wananchi waweze kujua namna huduma za kifedha zinavyotolewa na kampuni mbalimbali.
Wakati huohuo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetahadharisha wananchi kuhusu uwepo wa simu feki madukani.
Tahadhari hiyo ilitolewa na Kaimu Meneja Mawasiliano wa TCRA, Semu Mwakyanjala, katika maonesho hayo na kuwataka wananchi kuwa makini pindi wanaponunua simu.

Tuesday, October 9, 2012

CHADEMA yazindua kampeni za udiwani

UMATI mkubwa wa watu, juzi ulijitokeza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea udiwani wa kata ya Daraja Mbili wa Chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Prosper Msofe, uliofanyika kwenye mtaa wa Narvoi.
Aidha, viongozi wa chama hicho wakizungumza katika mkutano huo mbali ya kumuombea kura mgombea wao huyo, walitumia fursa hiyo kuutaka uongozi wa jiji la Arusha kuacha kufuata shinikizo la kisiasa katika kutafutia ufumbuzi suala la wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga kwa madai kuwa suala hilo ni kama bomu la muda linalosubiri kulipuka.
Pia waliitaka serikali kutoa majibu yanayoeleweka juu ya tukio la kutoroka kwa washtakiwa wawili wa kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA, kata ya Usa River, Msafiri Mbwambo, kwa madai kuwa kuna uwezekano nyuma ya mpango huo, kukawa na mkono wa wanasiasa ambao hawataki ukweli ujulikane.
Mwenyekiti wa wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro alisema inashangaza kuona halmashauri ya jiji la Arusha inaamua kuendesha shughuli zake kijima kwa kuamua kugawa uwanja wa NMC.
Nanyaro ambaye pia ni diwani wa Levelosi, aliuataka uongozi wa jiji la Arusha kushughulikia masuala yote kitaalamu kuepuka kuibua migogoro isiyo ya lazima kama ilivyo sasa ambapo licha ya machinga kupewa eneo lisilotosheleza kwenye uwanja wa NMC, lakini idadi ya waliokosa ni kubwa hivyo badala ya tatizo kupungua limeendelea kuongezeka.
Kwa upande wake, aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, alisema serikali isifanyie mzaha suala la watuhumiwa hao kutoroka, kwani lina utata mkubwa na pia linaacha maswali mengi kuliko majibu.
Kampeni hizo zinatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 28, mwaka huu ambapo zinawashirikisha wagombea kutoka vyama vya CCM na TLP.