Saturday, May 26, 2012

UKURASA WA KATIBA

Huu ni ukulisa utakao kutolea mfululizo wa ibara za katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ili kuendeleza suala la kuwasomesha na kuwajuza watanzania juu ya katiba yao inayoendelea kutumika sasa hususani katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye kutoa maoni kuhusu uundwaji wa katiba mpya ni matumaini yangu tutaifuatilia hatua kwa hatua palipo na swali au maoni usisite kuuliza kupitia dannymwakalindile2@gmail.com.
1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.
2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la
Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni
pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania
inapakana nayo.
(2) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali
ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika
mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibu
uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na
Bunge:
Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Rais
wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika
Mikoa, Wilaya au maeneo mengineyo.
Tangazo la nchi
yenye Mfumo wa
vyama vingi
3.-(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na
ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.
(2) Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshaji
wa vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii na ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa
ajili hiyo.
Utekelezaji wa
shughuli za
Mamlaka ya Nchi
4.-(1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuri
ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili
vyenye mamlaka ya utendaji, vyombo viwili vyenye mamlaka
ya kutekeleza utoaji haki, na pia vyombo viwili vyenye
mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa
shughuli za umma.
(2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni
Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki
vitakuwa ni Idara ya Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na Idara ya Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na
kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni
Bunge na Baraza la Wawakilishi.
(3) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma
katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa
madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa
katika ibara hii, kutakuwa na Mambo ya Muungano kama
yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza iliyoko

No comments:

Post a Comment