Kwa kweli elimu ya Tanzania imekuwa ya viwango vya chini sana, na suala hili lisipoangaliwa litalipeleka pabaya taifa hili. kimsingi elimu ya Tanzania imekuwa inaporomoka viwango kila siku ukilinganisha na kipindi cha selikari ya awamu ya kwanza, tatizo kubwa ni kwamba maendeleo ya elimu yamechukuliwa kama ni kujenga majengo na kusahau kuwa elimu ni zaidi ya majengo, elimu ni walimu, maabara, maktaba, na kadhalika.
miaka ya karibuni kumekuwa na mambo kadha yaliyofanyika ambayo ni ya maendeleo kwa elimu, mfano ujenzi wa shule za sekondari za kata, ni jambo zuri lakini mpango huo haukutanuliwa zaidi au haukusimamiwa ipasavyo,
wito kwa viongozi na wasimamizi wa miradi hii, ni mara mia tukafanya kitu mara moja ila kwa ubora kuliko kufanya kwa kulipualipua na kisha tukaja kurudia tena na tena.
No comments:
Post a Comment