Kila mmoja wetu aweza kushangazwa na hili kwa kuwa mara kwa mara mfumo dume umekuwa unamuonea mtoto wa kike hususani inapotukia kapewa mimba. huu mfumo dume unahistoria ndefu sana na umewatesa wanawake kwa muda mrefu sana, ulianza tangu enzi za mababu na mabibi zetu wa zamani, hawakuweza kusema kitu mbele ya mwanaume au wanaume, pia hawakuweza kurithi mali, na zaidi ya yote walilipiwa mali wakawekwa ndani kama mapambo ya nyumba hususani huko Zanzibar na Tanga. kwa hiyo si suala geni hata kidogo.
serikali inatakiwa kulifanyia kazi suala hili, yaani kwa suala la adhabu wapewe wote waliohusika hususani kama suala lenyewe linawagusa wanafunzi wa pande zote mbili, kwa upande waraia kuwapa mimba wanafunzi halina shaka kwani washitakiwa hufungwa jela miaka thelathini, lakini imekuwa ikitokea makubaliano yanafanyika kiholela baina ya wazazi na mtuhumiwa na kumaliza masuala hayo kienyeji, si vyema na mkondo au mwelekeo wa namna hii upigwe vita. kwa mawasiliano zaidi niandikie katika luisajohnson2011@yahoo.com
No comments:
Post a Comment