Saturday, May 5, 2012

ELIMU YA TANZANIA INAELEKE WAPI?

        kimsingi nimekuwa naguswa sana na hali ya elimu ya Tanzania kwa sasa, kwa kweli mambo yamekuwa yanaenda kombo kwa wanafunzi kila kukicha, suala hili limekuwa linawaathiri sana wanafunzi wanaohitimu Kidato cha nne kwani wamekuwa wanafanya vibaya sana katika masomo yao.
       sababu kubwa ya matokeo hayo ni kuingia kwa siasa mpaka kwenye suala la elimu, elimu imekuwa inaendeshwa kisiasa, hata kwa mambo ya msingi, wadau wa elimu wamekuwa wanaendeshwa sana na wanasiasa au wanasiasa wanafanya maamuzi bila kuwashirikisha wataalamu wa elimu matokeo yake ni kukwama kwa baadhi ya maadhimio, chukua mfano wa mabadiliko ya elimu ya miaka ya karibuni ya kufuta mitihani ya kidato cha pili na pia kuondoa masomo ya kilimo na biashara ni zo la maamuzi ya kisiasa bila kujali maamuzi ya kitaalamu kuhusu sekta ya elimu. matokeo yake ni nini inapotokea mitihani imeondolewa, au ikitokea hivyo mwanafunzi atasukumwa na nini wakati wanafunzi wetu hawana utamaduni wa kusoma? napenda kusemea sana suala hili ila kwa mwenye maoni zaidi anaweza kusema zaidi kwa kutoa maoni yake kwa ktumia anuani ya barua pepe luisajohnson2011@yahoo.com

No comments:

Post a Comment