Sunday, May 27, 2012
UKURASA WA KATIBA 2
5.-(1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka
kumi na minane anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi
unaofaywa Tanzania na wananchi. Na haki hii itatumiwa kwa
kufuata masharti ya ibara ndogo ya (2) pamoja na masharti
mengineyo ya Katiba hii na ya Sheria inayotumika nchini
Tanzania kuhusu mambo ya uchaguzi.
(2) Bunge laweza kutunga sheria na kuweka masharti
yanayoweza kuzuia raia asitumie haki ya kupiga kura kutokana
na yoyote kati ya sababu zifuatazo, yaani raia huyo-
(a) kuwa na uraia wa nchi nyingine;
(b) kuwa na ugonjwa wa akili;
(c) kutiwa hatiani kwa makosa fulani ya jinai;
(d) kukosa au kushindwa kuthibitisha au kutoa
kitambulisho cha umri, uraia au uandikishwaji kama
mpiga kura,
mbali na sababu hizo hakuna sababu nyingine yoyote
inayoweza kumzuia raia asitumie haki ya kupiga kura.
(3) Bunge litatunga Sheria ya Uchaguzi na kuweka
masharti kuhusu mambo yafuatayo-
(a) kuanzisha Daftari la Kudumu la Wapiga kura na
kuweka utaratibu wa kurekebisha yaliyomo katika
Daftari hilo;
(b) kutaja sehemu na nyakati za kuandikisha wapiga
kura na kupiga kura;
(c) utaratibu wa kumwezesha mpiga kura
aliyejiandikisha sehemu moja kupiga kura sehemu
nyingine na kutaja masharti ya utekelezaji wa
utaratibu huo;
(d) kutaja kazi na shughuli za Tume ya Uchaguzi na
utaratibu wa kila uchaguzi ambao utaendeshwa
chini ya uongozi na usimamizi wa Tume ya
Uchaguzi
Saturday, May 26, 2012
UKURASA WA KATIBA
Huu ni ukulisa utakao kutolea mfululizo wa ibara za katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ili kuendeleza suala la kuwasomesha na kuwajuza watanzania juu ya katiba yao inayoendelea kutumika sasa hususani katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye kutoa maoni kuhusu uundwaji wa katiba mpya ni matumaini yangu tutaifuatilia hatua kwa hatua palipo na swali au maoni usisite kuuliza kupitia dannymwakalindile2@gmail.com.
1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.
2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la
Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni
pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania
inapakana nayo.
(2) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali
ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika
mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibu
uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na
Bunge:
Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Rais
wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika
Mikoa, Wilaya au maeneo mengineyo.
Tangazo la nchi
yenye Mfumo wa
vyama vingi
3.-(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na
ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.
(2) Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshaji
wa vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii na ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa
ajili hiyo.
Utekelezaji wa
shughuli za
Mamlaka ya Nchi
4.-(1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuri
ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili
vyenye mamlaka ya utendaji, vyombo viwili vyenye mamlaka
ya kutekeleza utoaji haki, na pia vyombo viwili vyenye
mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa
shughuli za umma.
(2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni
Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki
vitakuwa ni Idara ya Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na Idara ya Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na
kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni
Bunge na Baraza la Wawakilishi.
(3) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma
katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa
madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa
katika ibara hii, kutakuwa na Mambo ya Muungano kama
yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza iliyoko

Thursday, May 10, 2012
mtoto wa kitaa Ibra mwampyate
Danny tolu ndani ya Forest mpya
IBRA Mwampyate a.ka. man calistussupa michael akionesha vitu vyake
kaka mwakalindile akitafakari jambo
hapo ni nyumbani simike mbeya jijini
mlima Rungwe, moja ya vivutio vya utalii wilayani Rungwe
kwa bibi TUKUYU
MAZOEZI MUHIMU, baadhi ya vifaa vya jgym mkwawa university
kaka umeuza gari lile umenunua hili?
abdala sambo upo wapi kwa sasa?
mkwawa university, iringa
bwana Danny
Tuesday, May 8, 2012
SUALA LA LAPTOP KWA KILA MWANACHUO
KILA MTU HAAMINI KAMA LINAWEZEKANA, LAKINI LINAWEZEKANA SUALA HILI, KWANI KAMA SUALA LA ELIMU BURE KWA SHULE ZA MSINGI LILIWEZEKANA NA PIA ADA YA 20000 KWA SHULE ZA SEKONDARI LIMEWEZEKANA IWEJE LAPTOP KWA KILA MWANACHUO LISIWEZEKANE?
TAZAMA RWANDA NCHI AMBAYO WAMEPIGANA VITA WENYEWE KWA WENYEWE KWA MUDA MREFU LEO HII WAMEMUDU LAPTOP KWA KILA MWANAFUNZI. TUJITAZAME VIZURI NA TUWEKE MIKAKATI YA KUWEZESHA SUALA HILO NDIPO MAFANIKIO YATAONEKANA.
KAMA UNAMAONI NIANDIKIE KATIKA EMAIL YANGU YA luisajohnson@yahoo.com

Sunday, May 6, 2012
ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA INAWEZEKENA!!!!!!
Kwa kweli elimu ya Tanzania imekuwa ya viwango vya chini sana, na suala hili lisipoangaliwa litalipeleka pabaya taifa hili. kimsingi elimu ya Tanzania imekuwa inaporomoka viwango kila siku ukilinganisha na kipindi cha selikari ya awamu ya kwanza, tatizo kubwa ni kwamba maendeleo ya elimu yamechukuliwa kama ni kujenga majengo na kusahau kuwa elimu ni zaidi ya majengo, elimu ni walimu, maabara, maktaba, na kadhalika.
miaka ya karibuni kumekuwa na mambo kadha yaliyofanyika ambayo ni ya maendeleo kwa elimu, mfano ujenzi wa shule za sekondari za kata, ni jambo zuri lakini mpango huo haukutanuliwa zaidi au haukusimamiwa ipasavyo,
wito kwa viongozi na wasimamizi wa miradi hii, ni mara mia tukafanya kitu mara moja ila kwa ubora kuliko kufanya kwa kulipualipua na kisha tukaja kurudia tena na tena.

Saturday, May 5, 2012
KWA NINI WATOTO WA KIKE WASIMAMISHWE MASOMO WANAPOPEWA MIMBA?
Kila mmoja wetu aweza kushangazwa na hili kwa kuwa mara kwa mara mfumo dume umekuwa unamuonea mtoto wa kike hususani inapotukia kapewa mimba. huu mfumo dume unahistoria ndefu sana na umewatesa wanawake kwa muda mrefu sana, ulianza tangu enzi za mababu na mabibi zetu wa zamani, hawakuweza kusema kitu mbele ya mwanaume au wanaume, pia hawakuweza kurithi mali, na zaidi ya yote walilipiwa mali wakawekwa ndani kama mapambo ya nyumba hususani huko Zanzibar na Tanga. kwa hiyo si suala geni hata kidogo.
serikali inatakiwa kulifanyia kazi suala hili, yaani kwa suala la adhabu wapewe wote waliohusika hususani kama suala lenyewe linawagusa wanafunzi wa pande zote mbili, kwa upande waraia kuwapa mimba wanafunzi halina shaka kwani washitakiwa hufungwa jela miaka thelathini, lakini imekuwa ikitokea makubaliano yanafanyika kiholela baina ya wazazi na mtuhumiwa na kumaliza masuala hayo kienyeji, si vyema na mkondo au mwelekeo wa namna hii upigwe vita. kwa mawasiliano zaidi niandikie katika luisajohnson2011@yahoo.com

ELIMU YA TANZANIA INAELEKE WAPI?
kimsingi nimekuwa naguswa sana na hali ya elimu ya Tanzania kwa sasa, kwa kweli mambo yamekuwa yanaenda kombo kwa wanafunzi kila kukicha, suala hili limekuwa linawaathiri sana wanafunzi wanaohitimu Kidato cha nne kwani wamekuwa wanafanya vibaya sana katika masomo yao.
sababu kubwa ya matokeo hayo ni kuingia kwa siasa mpaka kwenye suala la elimu, elimu imekuwa inaendeshwa kisiasa, hata kwa mambo ya msingi, wadau wa elimu wamekuwa wanaendeshwa sana na wanasiasa au wanasiasa wanafanya maamuzi bila kuwashirikisha wataalamu wa elimu matokeo yake ni kukwama kwa baadhi ya maadhimio, chukua mfano wa mabadiliko ya elimu ya miaka ya karibuni ya kufuta mitihani ya kidato cha pili na pia kuondoa masomo ya kilimo na biashara ni zo la maamuzi ya kisiasa bila kujali maamuzi ya kitaalamu kuhusu sekta ya elimu. matokeo yake ni nini inapotokea mitihani imeondolewa, au ikitokea hivyo mwanafunzi atasukumwa na nini wakati wanafunzi wetu hawana utamaduni wa kusoma? napenda kusemea sana suala hili ila kwa mwenye maoni zaidi anaweza kusema zaidi kwa kutoa maoni yake kwa ktumia anuani ya barua pepe luisajohnson2011@yahoo.com

Subscribe to:
Comments (Atom)